Lango la kuingia chumba maalum la maonyesho leo- limepambwa kwa wajihi wa bendera yetu na “dude” linaloonyesha aina ya mavazi yanayobuniwa na washoni hawa mahiri.
Maonyesho maarufu ya mavazi ya kimataifa –London Fashion Week- yatamega kitengo chake cha kimataifa kujenga washoni wapya toka Tanzania itakayofungua rasmi taa yake Ubalozi wetu leo Ijumaa mjini London.

Mto uliotandazwa kwa vazi maarufu la Kanga…maonyeshoni.
Mada ya maonyesho haya yatakayoendelea kwa juma zima ni “Swahili Flavour” (Ladha ya Kiswahili) na inategemea kutukuza kazi za Watanzanua kupitia wabunifu mavazi ni Christine Mhando (anayejiita “Chichia London”) na Anna Lukindo anayetumia jina la “Anna Luks.”

Anna Luks
Christine Mhando alihitimu chuo cha Usanii cha Kent mwaka 2002 na huhimiza mtindo wa Kanga kama wajihi wa kazi zake, ilhali Anna Luks mhitimu wa chuo cha Middlesex, London anayo fani ya kamba kamba, mavazi ya kike na usasa unaotawala ubunifu wake.

Wote wanasema wana lengo la kukuuza utamaduni wa Kitanzania, kutangaza taswira za Kiswahili na sura mbalimbali za Afrika Mashariki. Pamoja nao wasanii hawa ni msaidizi wao–ambaye bado anasomea upambaji mavazi, Margaret Waiyego – mzawa wa Kenya.

Margaret Waiyego, mwanafunzi anayesaidia kazi hii kwa kujitoleaKaimu Balozi wetu London, Mheshimiwa Chabaka Kilumanga alisema jana kwamba maonyesho haya ya kimataifa yatakua nafasi kubwa kwa Tanzania kujenga jina lake na ni sehemu mahsusi ya kujivunia utamaduni asilia. Shirika la maendeleo ya utamaduni na elimu British Council ndiye mgharamiaji wa shughuli hii yenye lengo la kujenga vipaji na kazi za mavazi za washoni wasiofahamika duniani.

Lango la kuingia chumba maalum la maonyesho leo- limepambwa kwa wajihi wa bendera yetu na “dude” linaloonyesha aina ya mavazi yanayobuniwa na washoni hawa mahiri.
Maonyesho maarufu ya mavazi ya kimataifa –London Fashion Week- yatamega kitengo chake cha kimataifa kujenga washoni wapya toka Tanzania itakayofungua rasmi taa yake Ubalozi wetu leo Ijumaa mjini London.

Mto uliotandazwa kwa vazi maarufu la Kanga…maonyeshoni.
Mada ya maonyesho haya yatakayoendelea kwa juma zima ni “Swahili Flavour” (Ladha ya Kiswahili) na inategemea kutukuza kazi za Watanzanua kupitia wabunifu mavazi ni Christine Mhando (anayejiita “Chichia London”) na Anna Lukindo anayetumia jina la “Anna Luks.”

Anna Luks
Christine Mhando alihitimu chuo cha Usanii cha Kent mwaka 2002 na huhimiza mtindo wa Kanga kama wajihi wa kazi zake, ilhali Anna Luks mhitimu wa chuo cha Middlesex, London anayo fani ya kamba kamba, mavazi ya kike na usasa unaotawala ubunifu wake.

Wote wanasema wana lengo la kukuuza utamaduni wa Kitanzania, kutangaza taswira za Kiswahili na sura mbalimbali za Afrika Mashariki. Pamoja nao wasanii hawa ni msaidizi wao–ambaye bado anasomea upambaji mavazi, Margaret Waiyego – mzawa wa Kenya.

Margaret Waiyego, mwanafunzi anayesaidia kazi hii kwa kujitolea

Tags:
Business