KOCHA wa Taifa Stars, Kim Poulsen amesema haoni sababu kwa nini kikosi chake kishindwe kucheza fainali zijazo za Kombe la Mataifa ya Afrika zitakazofanyika mwaka 2015.
Mara ya mwisho Stars kushiriki fainali hizo ilikuwa miaka 33 iliyopita nchini Nigeria, ambapo ilitolewa hatua ya makundi, ikitoka sare moja na kufungwa mbili.
“Tumecheza mechi ya kirafiki dhidi ya Zambia na Ethiopia kama sehemu ya maandalizi ya kuhakikisha Stars itakuwa miongoni mwa zile zitakazocheza Afcon 2015,” alisema Poulsen.
“Tutacheza kwa staili yetu kwa sababu ni sehemu ya maandalizi kabla ya mechi ya Morocco. Wachezaji wameonyesha kiwango kizuri,” alisema wakati akitaja majina ya mastaa watakaounda Stars kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Cameroon.
Mchezo huo unatarajia kupigwa Jumatano kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam na Poulsen anatarajia kikosi chake kitafanya vizuri.
Kim alirejea nchini juzi akitoka Afrika Kusini alikokwenda kuzipeleleza timu za Morocco na Ivory Coast ambazo ziko kundi moja na Tanzania katika mechi za mchujo kusaka tiketi ya kucheza Kombe la Dunia.
Kuhusu kikosi chake, Poulsen alisema amemwacha John Bocco kutokana na kuwa majeruhi na Amir Maftah, ambaye hajamshuhudia akicheza hivi karibuni.
Alisema katika kikosi chake amewaita Erasto Nyoni na Aggrey Morris japo wachezaji hao wanatuhumia kujihusisha na rushwa na suala lao liko Takukuru.
Wengine walioitwa ni makipa Juma Kaseja (Simba), Mwadini Ally na Aishi Manula (Azam).
Mabeki: Erasto Nyoni (Azam), Nassoro Cholo (Simba), Aggrey Morris (Azam), Nadir Haroub (Yanga), Kelvin Yondani (Yanga), Shomari Kapombe (Simba) na Issa Rashid (Mtibwa Sugar).
Viungo: Amri Kiemba (Simba), Simon Msuva (Yanga), Frank Domayo (Yanga), Shabani Nditi (Mtibwa Sugar), Salum Abubakar (Azam), Khamis Mcha (Azam), Athuman Idd (Yanga) na Mwinyi Kazimoto (Simba).
Washambuliaji: Mrisho Ngasa (Simba), Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe) DRC.Kikosi hicho kinatarajiwa kuingia kambini Jumapili jioni.