KAMPUNI YA VODACOM KUPITIA HUDUMA YAKE YA M-PESA KUPUNGUZA FOLENI KATIKA MABENKI


001.m-pesa e403c
Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim (katikati) akitoa elimu kwa wateja wa Benki ya Posta Tanzania tawi la Msimbazi jijini Dar es salaam kuhusu huduma inayowawezesha wateja wa Benki hiyo kuweka na kutoa fedha zao kutoka kwenye akaunti ya Benki hiyo kupitia simu za mkononi kwa njia ya M-pesa. Kulia ni Meneja wa Tawi hilo Maduhu Makoye.Huduma hiyo inapatikana pia kwa wateja wa mabenki mbalimbali nchini na kuweza kupunguza msongamano wa foleni katika mabenki.


Uwepo wa huduma ya M-pesa nchini ni wazi sasa unazidi kuwa wa manufuaa zaidi kwa kada zote za wananchi ambapo sasa wateja wa benki mbalimbali za biashara nchini hawana sababu ya kuingia gharama wala kusimama katika foleni kwa ajili ya kuweka ama kutoa fedha katika akaunti zao kwa kuwa hilo sasa linaweza kufanyika kupitia kiganja cha mkono.
Hali hiyo inafuatia huduma ya M-pesa kuungana na mabenki mbalimbali nchini ili kuwawezesha wateja wa mabenki hayo kuweza kuweka na kuchukua fedha kutoka katika akaunti zao kupitia simu ya mkononi kwa njia ya M-pesa. Huduma hii tayari inapatikana kwa benki kadhaa za biashara hapa nchini. 
Akizungumza wakati wa zoezi la kutoa elimu kwa wateja wa Benki ya Posta Tanzania Tawi la Msimbazi jijini Dar es salaam, Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania Salum Mwalim amesema hatua hiyo iliyofikiwa ni mwendelezo wa azima ya Vodacom ya kuongeza kasi katika ubunifu kwa lengo la kuyafanya maisha ya wananchi kuwa mepesi na yasiyo na gharama.
“Siku zote tunaangalia ni kwa namna gani tunatumia teknolojia ya simu za mkononi kuyafanya maisha ya watu kuwa rahisi na mepesi zaidi ili kuwapunguzia gharama za maisha, ni wazi kwamba hii ni hatua nyengine muhimu ya kwanza kutoka Vodacom.”Alisema Mwalim
Mwalim amesema katika zama hizi ambazo dunia imekuwa ikishuhudia ukuaji wa kasi wa idadi ya watu huku rasilimali zikiwa haba njia mojawapo muhimu inayoweza kusaidia ulimwengu kupunguza pengo hilo ni kuwa na teknolojia zinazoweza kutumiwa huku zikipunguza matumizi ya rasilimali nyengine katika jambo moja.
Mwalim amesema kasi ya ubunifu inayoonyeshwa na M-pesa ni sababu mojawapo ya watanzania kujivunia kuwepo kwa huduma hiyo ya fedha kwa njia ya simu ya mkononi inayoongoza nchini na kuendelea kuiunga mkono kwa kuelewa fursa zilizomo ndani yake na kuzitumia kwa ufasaha na ufanisi ili kunufaika nazo.
“Leo hii hakuna haja hata kidogo ya kuingia gharama za usafiri na muda kwa kufuata tawi la Benki na kupanga foleni kwa jambo ambalo mteja wa Benki anaweza kupiga *150*00# katika simu yake ya mtandao wa Vodacom iliyosajiliwa na M-pesa na kuunganishwa na Menu ya M-pesa na hapo anaweza kufanya kile ambacho kingemlazimu kukifuata katika tawi la Benki husika kwa gharama kubwa.” Aliongeza Mwalim
Mwalim aliongeza kuwa “Hakuna sababu ya watanzania kuogopa kutumia teknolojia, na huu ni wakati ambao kuwa na simu iliyounganishwa na mtandao unaaongoza wa Vodacom na kusajiliwa na huduma  salama, ya kuaminika  na ya uhakika ya M-pesa ni jambo lenye thamani na umuhimu wa kipekee katika maisha ya kila mmoja.”
Kwa upande wake Meneja wa Tawi hilo Maduhu Makoye amesema kuja kwa huduma hiyo kutawawezesha wateja wa benki hiyo kuwa na urahsi zaidi katika kupata huduma za kibenki hata kule ambako huduma hizo bado hazijafika.
“Kupitia huduma hii ya kuweka na kuchukua fedha kupitia M-pesa tutawafikia wateja wengi zaidi, na tutwapunguzia wateja wetu usmbufu wa kupanga foleni.”Alisema Makoye na kuongeza “Tunawaomba wateja wetu kutumia njia ya M-pesa kuweka na kuchukua fedha, huu ubia wenye faida kubwa hasa kwa wananchi ambao bado hawajafikiwa na huduma za kibenki kwani sasa wanawaeza kuwa wateja wa Benki yetu na kufurahia huduma kwa urahisi kupitia M-pesa.”
Mbali na Benki ya Posta Tanzania huduma kama hiyo inapatkiana pia katika mebenki ya CRDB,BOA, AMANA, NMB,Standard Chartered, Access Bank, Akiba, DTB na Banc ABC
Mbali na kuwawezesha wateja wake kuweza kuweka na kuchukua fedha kutoaka akaunti za benki hizo, M-pesa pia inawawezesha wateja wake kulipia huduma mbalimbali ikiwemo kunua LUKU,tiketi za usafiri wa anga kulipia Dawsco, DSTV, StarTimes miongoni mwa huduma nyingi ambazo M-pesa huwaunganisha wateja wake. 
Previous Post Next Post