FAINALI AFCON: BURKINA FASO NI ' GANDA LA NDIZI!'


8 d2ce6

Nigeria, Nigeria, Nigeria...!
Wapenzi wengi wa soka wanaizungumzia Nigeria, lakini, wengi hao wanaweza kuwa kwenye upande usio sahihi wa reli ya soka.
Burkina Faso nimewafuatilia tangu mwanzo wa mashindano. Naweza kusema hiki; kuwa ndio walio na ' Momentum' kwa sasa. Timu kupata momentum ina maana kama vile gari inavyoanza kushika kasi baada ya kuanza taratibu. Na Momentum waliyo nayo Burkina Faso kwa sasa ni kama ilivyokuwa kwa Chipolopolo Afcon iliyopita.
Wa- Burkinabe wamekwenda Afcon ya mwaka huu wakionekana kama ' Outsiders'- Hawakuhesabiwa. hawajawahi kucheza fainali za Afcon. Hawana cha kupoteza na hii ni fursa yao ya kihistoria, na upepo uko upande wao- Momentum.
Kumbuka, hatua ya makundi walitoka sare na Nigeria na Ghana, wakawafunga Ethiopia. Na kundi lao ndilo lilikuwa ' Kundi la Kifo'.
Nigeria watacheza kwa shinikizo. Nigeria ni timu iliyo na nyota wengi, na pengine huo utakuwa ni udhaifu wao. Huenda wakaidharau Burkina Faso. Itakuwa ni sawa na lulidharau  ganda la ndizi. Katika maisha,mwanadamu unaweza kuangushwa na ganda la ndizi. Maana, usipokuwa makini na ganda la ndizi, kulikanyaga itakuwa na maana ya kuteleza na kuanguka.
Usiku wa leo ulimwengu wa soka ujiandae na ' Maajabu' mengine ya soka; kwamba Burkina Faso inaweza kuibuka mabingwa. Na tusubiri tuone.

Bongo 61
Dar es salaam.
0716 851 958
Previous Post Next Post