CHADEMA DODOMA WALALAMIKIA TATIZO LA MIKUTANO


bungee 75bca

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Dodoma  imesema kuwa agozi la Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkr Rehema Nchimbi la kukataza mikutano,maandamano na midahalo ya vyama vya siasa katika kipindi cha vikao vya Bunge.
Agizo hilo ni kuvunja sheria namba 5 ya vyama vya siasa ya mwaka 1992 na sheria ya Jeshi la Polisi linalosimamia uendeshaji wa shughuli za yama vya siasa nchini,

Tamko hilo limetolewa na  Katibu wa Chadema Mkoa wa Dodoma Stephen Masaawe  kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari mjini hapa.
Katibu huyo wa Chadema alisema kuwa agizo la Mkuu wa Mkoa wa Dodoma  alilolitoa lina madhara makubwa kwa jamii na alitakiwa alifikishe kwenye mkutano kwa wadau ili kujadili hatua za kuchukua na siyo hivyo alivyofanya.
''Mkuu  wa mkoa kama alihitaji Sheria hiyo namba 5 ya vyama vya Siasa ifanyiwe     marekebisho  kwa ajili ya mkoa wa Dodoma,angeshauri serikali kupeleka mswaada huo bungeni kwa ajili ya mkoa huu na si vinginevyo'', alisema
Aidha Massewe alisema kutokana na tamko hilo Chadema Mkoa wa Dodoma  kinamtaka msajili wa vyama vya siasa nchini,kutambua kwamba kamwe agizo hilo halitatekelezwa  kwa sababu za kuwepo kwa uvunjifu wa sheria  hiyo ambayo ilitungwa na Bunge mwaka 1992.
“Kwa tamko hilo la Mkuu huyo wa Mkoa tunapenda kuweka wazi na kujulisha kuwa Chadema Mkoa wa Dodoma kamwe hatutatii agizo hilo kwa sababu aliyetoa ni mkuu wa mkoa na siyo msajili wa vyama vya siasa.”Massawe alisema.
Katibu Massewe akisisitiza katika tamko hilo alisema kuwa tangu mwaka 1992 ilipotungwa sheria ya Bunge imeendelea kukutana Dodoma na mikutano,maandamano na midahalo haikuweza kusitishwa kwa kipindi hicho.
Alisema hisia za Mkuu huyo wa Mkoa wa Dodoma haziwezi kuwa sababu ya kuvunja sheria  ya vyama vya siasa,na kwa jinsi hiyo hana mamlaka yeyote kuhusu ufanyikaji wa maandamano,mikutano na midahalo la sivyo sheria hiyo ifutwe ndipo atangaze anavyota.
Mwaka 2012 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt Rehema Nchimbi alizuia mikutano yote ya vyama vya siasa kufanyika katika mkoa wa Dodoma katika kipindi kinachofanyika mikutano ya Bunge.

Previous Post Next Post