WATU 230 WAFARIKI DUNIA UKO BRAZIL



Mji wa Santa Maria
WATU zaidi ya 232 wamefariki kwenye ajali ya moto uliozuka katika ukumbi ya starehe uliopo mjini Santa Maria, katika jimbo la Rio Grande do Sul, nchini Brazil.
Kwa mujibu wa idara ya zima moto mjini humo moto huo ulizuka muda wa saa nane usiku kutokana na maonyesho ya fataki yaliyorushwa wakati wa tamasha lililoandaliwa na kuhudhuriwa na wanafunzi kutoka chuo kikuu kilichopo karibu.
Waliongeza kuwa timu za uokozi zilifanya kila juhudi wakishirikiana na Meya wa mji wa Santa Maria, Cleberson Bastianello kwa ajili ya kuzitafuta maiti hizo katika klabu hiyo iliyojulikana kwa jina la Kiss.
Katika juhudi hizo za uokozi, jumla ya watu 131 walionekana wakiwa na majeraha hali iliyosababisha kulazwa hospitalini kwa ajili ya matibabu zaidi.
Idadi kubwa ya watu waliokufa ilitokana na kukosa hewa kwa muda mrefu jambo ambalo lilisabaisha kushindwa kupumua na hatimaye kufariki.
Awali polisi walisema idadi ya watu waliokufa ilikuwa 245 lakini taarifa za mwisho zilisema kuwa watu waliofariki walikuwa ni 232.
Kutokana na vifo hivyo Rais wa nchi hiyo , Dilma Rousseff, alilazimika kukatiza ghafla kushiriki kwenye mkutano kati ya Umoja wa Ulaya na nchi za Amerika kusini mjini Santiago, Chile na kurejea Santa Maria.
Previous Post Next Post