Mjumbe wa Sekretarieti ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Bi. Hanifa Masaninga akitoa ufafanuzi kuhusu uandaaji wa maoni ya wananchi na kuwa Kitengo cha Taarifa Rasmi (Hansard) kwa ujumbe wa Taasisi za Habari nchini waliotembelea ofisi za Tume leo (januari 10, 2013). Taasisi zilizotembelea Tume ni Baraza la Habari Tanzania (MCT), Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari (MOAT), Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA) na Jukwaa la Wahariri (TEF).