Afisa Habari Ngazi ya Taifa wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi. Usia Nkoma akisoma ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon katika Siku ya Kimataifa ya Kuwakumbuka wahanga wa Mauaji ya Kimbari ya Holocaust kwa vijana wanafunzi wa shule za sekondari na baadhi ya vyuo.
Amesema katika siku hii ya kimataifa, tuwakumbuke watu wote wasio na hatia ambao walipoteza maisha wakati mauaji ya kimbari ya Holocaust.
Ameongeza kuwa vilevile tuhamasishe na wale ambao walikuwa na ujasiri wa kujali watu wa kawaida ambao walichukua hatua zisizo za kawaida kulinda heshima ya binadamu. Mfano wao unaweza kutusaidia sisi kujenga dunia bora zaidi leoKauli mbiu ya mwaka huu ni “Uokoaji wakati wa Mauaji ya Kimbari: Ujasiri wa Kujali”.
baadhi ya Wanafunzi wa shule za sekondari na vyuo wakimsikiliza kwa makini Bi. Usia Nkoma (hayupo pichani) alipokuwa akisoma ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa wakati wa Siku ya Kimataifa ya Kuwakumbuka wahanga wa Mauaji ya Kimbari ya Holocaust iliyofanyika jijini Dar leo katika ukumbi wa British Council.