MOAT NA TEF NAO WATOA MAONI KATIBA MPYA


media1 256feMwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Bw. Absolom Kibanda akimkabidhi maoni ya Jukwaa hilo kuhusu katiba Mpya Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Prof. Mwesiga Baregu katika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam leo  (Alhamisi, Jan 10, 2013) .

media2 30d2d
Mwanachama wa Jukwaa la Wahariri (TEF) Bw. Deodatus Balile akiwasilisha maoni ya Jukwaa hilo kuhusu Katiba Mpya katika mkutano uliofanyika katika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam leo  (Alhamisi, Jan 10, 2013). Wengine ni Bw. Ruge Mutahaba (kushoto) kutoka Clouds Media Group na Bw. Yasin Sadik kutoka gazeti la Hoja.
media3 bf204
Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) Bw. Kajubi Mukajanga akiwasilisha maoni ya Baraza hilo kuhusu Katiba Mpya katika mkutano uliofanyika katika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam leo  (Alhamisi, Jan 10, 2013). Kulia ni Bi. Pili Mtambalike kutoka MCT.
media 8f4b3
Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari (MOAT) Bw. Reginald Mengi akitoa maoni ya chama hicho kuhusu Katiba Mpya katika mkutano na Tume ya Mabadiliko ya Katiba leo (Alhamisi, Jan 10, 2013) katika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mjumbe wa Tume hiyo Prof. Palamagamba Kabudi.
Previous Post Next Post