Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Iringa akizungumza na baraza la madiwani hawako pichani.
Na Denis Mlowe – IringaKiasi cha shilingi milioni 215 kutumika katika ujenzi wa madarasa, nyumba za walimu na vyoo katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Vijijini.
Hayo yamesemwa na Afisa Elimu wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Seleman Pandawe wakati akizungumza mbele ya baraza la madiwani katika kikao maalum cha kamati ya fedha, mipango na utawala na baraza la madiwani kwa lengo la kupokea na kujadili na kupitisha rasimu ya mpango bajeti ya halmashauri ya Wilaya kwa mwaka 2013/ 2014 kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Siasa ni Kilimo.Alisema kwamba Ujenzi huo utaokaokamilika mwezi Juni mwaka 2014 utazinufaisha shule za zilizoko katika Wilaya hiyo na fedha hizo zimetokana na mapato ya ndani na nyingine kutoka Serikalini kwa mpango wa fedha wa bajeti ya 2013/ 2014.Pandawe alizitaja shule 20 ambazo zitanufaika na ujenzi wa madarasa ni shule za Ng’enza, Idodi, Ilolo Mpya, Ikengeza, Kinyika,Mkombe,Mfyome, Chamgogo, Matalawena na Makadufu aidha aliongeza kusema shulre nyingine ni Ukombozi, Mwanyengo, Kidilo,Kiwewe, Makuka, Lumuli, Mkomilenga, Sasamambo na Nyakavangala.Nyumba za walimu zitajengwa katika shule za Kidilo, Ukombozi, Makadupa, Nyamihuu, Mlanda,Mbuyuni,Kalenga, Kihanga, Kinyali na Kitanewa na ujenzi wa vyoo vya vyenye matundu 50 utazinufaisha shule za Ihomba itakayopata matundu 30 na shule ya Kinywang’anga watapata matundu 20.
Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Iringa akizungumza na baraza la madiwani hawako pichani.
Na Denis Mlowe – Iringa
Kiasi cha shilingi milioni 215 kutumika katika ujenzi wa madarasa, nyumba za walimu na vyoo katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Vijijini.
Hayo yamesemwa na Afisa Elimu wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Seleman Pandawe wakati akizungumza mbele ya baraza la madiwani katika kikao maalum cha kamati ya fedha, mipango na utawala na baraza la madiwani kwa lengo la kupokea na kujadili na kupitisha rasimu ya mpango bajeti ya halmashauri ya Wilaya kwa mwaka 2013/ 2014 kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Siasa ni Kilimo.
Alisema kwamba Ujenzi huo utaokaokamilika mwezi Juni mwaka 2014 utazinufaisha shule za zilizoko katika Wilaya hiyo na fedha hizo zimetokana na mapato ya ndani na nyingine kutoka Serikalini kwa mpango wa fedha wa bajeti ya 2013/ 2014.
Pandawe alizitaja shule 20 ambazo zitanufaika na ujenzi wa madarasa ni shule za Ng’enza, Idodi, Ilolo Mpya, Ikengeza, Kinyika,Mkombe,Mfyome, Chamgogo, Matalawena na Makadufu aidha aliongeza kusema shulre nyingine ni Ukombozi, Mwanyengo, Kidilo,Kiwewe, Makuka, Lumuli, Mkomilenga, Sasamambo na Nyakavangala.
Nyumba za walimu zitajengwa katika shule za Kidilo, Ukombozi, Makadupa, Nyamihuu, Mlanda,Mbuyuni,Kalenga, Kihanga, Kinyali na Kitanewa na ujenzi wa vyoo vya vyenye matundu 50 utazinufaisha shule za Ihomba itakayopata matundu 30 na shule ya Kinywang’anga watapata matundu 20.