MANCHESTER UNITED YAWEKA REKODI YA KUWA TIMU YA KWANZA YENYE THAMANI YA DOLA BILLIONI 3



Manchester United imekuwa timu ya kwanza ya michezo duniani kuwa na thamani ya $3 Billion kwa mujibu wa jarida la biashara la kimarekani la Forbes.

United wameshika nafasi ya kwanza mbelel ya timu ya soka la kimarekani yaDallas Cowboys, yenye thamani ya $2.1bn.
Kwa mujibu wa Forbes: ‘Pamoja na kushuka kwa mapato kipindi cha miezi kadhaa iliyopita kutokana na mapato kutoka kwenye TV kushuka, lakini thamani ya hisa za mabingwa wa 19 wa England imepanda kutokana mikataba mikubwa ya kibiashara ambayo timu hiyo imeingia na kampuni za Kansai, Benji ya Ujenzi ya China, huku kukiwa na mweleko wa kupata mafanikio kwenye ligi kuu ya England pia mapato ya Champions League.

Hisa za klabu hiyo ya Old Trafford zilifanya vibaya sokoni zilipotolewa hadharani mnamo mwezi wa nane mwaka jana, lakini sasa hali imebadilika na kuwa nzuri kwenye hisa hizo baada ya klabu hiyo kuingia mikataba mingi ya kibiashara na makampuni tofauti.

Wakati huo huo, Manchester City wapo karibuni kuchukua nafasi ya pili kuwa timu ya pili ya EPL inayoongiza fedha ikiwapita watoto wa London Chelsea na Arsenal.

City wameingiza fedha nyingi kuliko Spurs na Liverpool baada ya kushinda ubingwa, na kama wataendelea kupata mafanikio haya ndani ya kipindi cha miezi 24 ijayo kwa hakika wanatajwa kuwa nyuma ya United badala ya Arsenal na Chelsea.


HII NDIO LISTI YA TIMU ZILIZOINGIZA FEDHA NYINGI MWAKA 2011-12 KWA MUJIBU WA DELOITTE 

1 Real Madrid - £414.7m (revenue 2011-12)
2 Barcelona - £390.8m
3 Manchester United - £320.3m
4 Bayern Munich - £298.1m
5 Chelsea - £261m
6 Arsenal - £234.9m
7 Manchester City - £231.1m
8 AC Milan - £207.9m
9 Liverpool - £188.7m
10 Juventus - £158.1m
11 Borussia Dortmund - £153m
12 Inter - £150.4m
13 Tottenham - £144.2m
14 Schalke - £141.2m
15 Napoli - £120.1m
16 Marseille - £109.8m
17 Lyon - £106.7m
18 Hamburg - £98m
19 Roma - £93.8m
20 Newcastle - £93.3m
Previous Post Next Post