Keshi awatema wachezaji wanne

Kocha wa Nigeria Stephen Keshi

Kocha wa Nigeria Stephen Keshi, amewaacha nje wachezaji wanne, katika kikosi chake kitakachoshiriki katika fainali ya kombe la Mataifa ya Afrika.
Rabiu Ibrahim anayeichezea klabu ya Kilmarnock, Papa Idris wa Kano Pillars, Henry Uche wa Enyimba na Uche Kalu, anayecheza soka ya kulipwa nchini Uturuki ambaye amejeruhiwa waliondolewa kwenye kikosi hicho kinachojiandaa nchini Ureno.
Kocha huyo pia amekubali kuwa mlinda lango wa Millwall, Danny Shittu na Shola Ameobi wa Newcastle pia hawatashiriki katika fainali hizo.
Ibrahim aliondolewa katika timu hiyo ya taifa ta Nigeria baada ya kufika kambini akiwa amechelewa na pia hakupata nafasi ya kuichezea klabu yake ya Celtic mapema na hivyo, kuwa katika hali mbaya.
Kufuatia tangazo hilo, Ibrahim sasa aweza kuendelea na mikakati yake ya kutafuta matumaini yake ya kuwa miongoni mwa wachezaji kumi na mmoja wa kwanza wa Celtic baada ya kuichezea klabu ya Sporting Lisbon, PSV Eindhoven na Celtic.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 alijiunga na Kilmarnock, kutoka klabu ya Celtic wiki iliyopita baada ya kushindwa kupata nafasi ya kucheza katika klabu hiyo.
Previous Post Next Post

Popular Items