STAA wa Bongo anayetesa kwenye mitindo, Jacqueline Patrick anakabiliwa na msala wa kumtwanga na chupa nusu kumuua mrembo anayejulikana kwa jina la Hafsa Sasya
Habari zilizopenyezwa na chanzo chetu kutoka eneo la tukio zinasema kwamba, ishu ilitokea usiku wa kuamkia Jumamosi ya Januari 26, mwaka huu ndani ya Ukumbi wa Elements Lounge uliopo Masaki, Dar.
Jack alifikishwa Kituo cha Polisi Oysterbay na kufunguliwa kesi yenye jalada namba OB/RB/1678/13 KUJERUHI.
KAULI ZAO :
KAULI YA JACK
“Ni kweli kulitokea ugomvi siku ile...na ni kweli nilihojiwa na Polisi wa Kituo cha Oysterbay, lakini nimetoka kwa dhamana na kesi imekwenda mahakamani.”
KAULI YA HAFSA
“Mimi na Jack tulikuwa marafiki lakini nashangaa amenipiga na chupa bila sababu. Nimeshonwa nyuzi tatu. Siku ile alinikuta nimesimama na rafiki yangu mara akanipiga kikumbo kisha akaenda chooni, aliporudi akanikumba tena, nilipomuuliza ikawa kosa; akanipiga na chupa.
“Imeniuma sana maana amenipa jeraha usoni mwangu bila sababu ya msingi, maana sina ugomvi naye. Kwa sababu hili suala lipo mikononi mwa sheria, naamini itachukua mkondo wake.”