Nchi za Uganda na Sudan Kusini zimetiliana saini mkataba wa kuimarisha ushirikiano wa kisiasa na kuisalama ikiwa ni njia ya kuboresha amani.
Makubaliano hayo ambayo pia yamezungumzia kushirikiana katika Nyanja za fedha, biashara, utalii, elimu na ushuru yametiwa saini jijini Kampala.
Waziri wa Nchi wa masuala ya Kimataifa wa Uganda Okello Oryem ametia saini mkataba huo kwa niaba ya serikali yake wakati Waziri wa Mambo ya Nje wa Sudan Kusini Nhial Deng Nhial amesaini kwa niaba ya nchi yake.
Sudan Kusin imeshauriwa kuomba kujiunga na Mamlaka ya Nile Basin, ambayo inazikutanisha pamoja nchi zilizopo katika Nila Basin, ambapo chini ya ushirikiano na Uganda, pamoja na mambo mengine nchi hizo mbili zitaweza kufanya mashauriano ya pamoja juu ya mipaka na kuweka mipaka hiyo.