Mh. Mama Salma Kikwete akihutubia katika uzinduzi wa chanjo mpya katika kituo cha afya Buguruni ambapo amesema Idadi ya magonjwa yanayokingwa kwa chanjo imeendelea kuongezeka kutoka manne hadi tisa kufikia 2009 na kuwa chanjo inayozinduliwa itafanya maradhi yanayokingwa kwa chanjo kufikia 11.
 Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hussein Mwinyi akisoma hotuba yake.
Baadhi ya Kinamama na watoto wao waliojitokeza katika uzinduzi wa Chanjo hizo.
Mama Salma Kikwete akitoa chanjo kwa mmoja wa watoto kuashiria uzinduzi wa chanjo mpya za “PVC 13 na Rotarix” kukinga watoto dhidi ya Nimonia na magonjwa ya kuhara.
Mjomba band yaa Mrisho Mpoto ikitoa burudani wakati wa uzinduzi wa chanjo ya watoto.
Wasanii wa Mjomba band wakiserebuka katika hafla hiyo.
Pichani Juu na Chini baadhi ya wadau wa sekta ya Afya, Wananchi na Maafisa wa Wizara ya Afya katika uzinduzi huo.
Na. MO BLOG TEAM
Tanzania kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii leo imezindua chanjo mpya zinazolenga kukinga watoto dhidi ya nimonia na magonjwa ya kuhara yanayo sababishwa na kirusi cha Rotavirus.
Akizindua chanjo hiyo leo Mke wa rais Mama Salma Kikwete amesema kirusi cha Rotavirus kinachangia asilimia 18 ya vifo vya watoto vinavyotokana na kuharisha.
Amesema kuongezeka kwa chanjo hizi hapa nchini kutapunguza vifo vya watoto vitokanavyo na maradhi haya ili kufikia lengo la mileni namba 4 ifikapo 2015.
Aidha Mama Salma ametoa rai kwa wananchi kuendeleza juhudi mbalimbali za kuboresha afya ikiwa ni pamoja na kunawa mikono kwa nyakati muhimu hususan kabla ya kula au kuandaa chakula, pia baada ya kujisaidia.