SAM WA UKWELI AKAMILISHA SAMAKI



video ya kibao kipya cha msanii Sam wa Ukweli iitwayo 'Samaki' imekamilika na itaanza kuonekana kwenye televisheni hivi karibuni

Akizungumza jijini msanii huyo alisema video hiyo imechukuliwa picha zake sehemu mbalimbali nchini  na ni video ambayo mashabiki wengi wataipenda kuiona

Alisema pia video hiyo imetengenezwa kwa kiwango chenye ubora wa hali ya juu na pia wataalamu wa kuchanganya rangi wamefanya kazi nzuri ambayo mashabiki wataikubali pale watakapoiona ikichezwa kwenye televisheni
Previous Post Next Post