Mulenga kuhamia England


Jacob Mulenga
Jacob Mulenga

Mshambulizi wa timu ya taifa ya Zambia, Jacob Mulenga anasema yuko tayari kusajiliwa na klabu moja inayoshiriki katika ligi kuu ya Premier ya England.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28, ni mchezaji aliyefunga idadi kubwa ya magoli na klabu yake ya Utrecht.
Mchezaji huyo amesema babake ambaye alifariki mapema mwaka huu, alimshauri kutafuta klabu inayoshiriki ligi ya England.
Mwezi agosti mwaka huu mshambulizi mwingine wa Zambia, Emmanuel Mayuka, alisajiliwa na klabu ya Southampton.
Mlinda lango wa timu hiyo ya Chipolopolo, Stophilla Sunzu amehusishwa na ligi ya England.
Previous Post Next Post