MSANII RICH MAVOCAL AWASHUKURU WADAU WA MUZIKI


Msanii  Richard  Lusinga (a.k.a – Richie Mavoko) akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani Dec,28,2012 jijini Dar es Salaam, wakati akitoa shukrani kwa niaba ya  Kampuni yake ya Aljazerra Entertaiment,  katika shukurani zake amesema,” kama msanii wa kizazi kipya  amewomba radhi  kwa wote  aliowakosea na yeye pia amewasemehe” Pamoja na Kushukuru kampuni ya Aljazerra Entertaiment, waandishi wa habari na wadau wote wa muziki nchini, kwani ndio  waliomfikisha hapo alipofikia na kuahihidi atazidi kuboresha na kuwaletea  nyimbo kali zaidi washabiki wake katika mwaka wa 2013.Richie Mavoko anatamba na nyimbo zake kama Mbona silai,Folo folo me,one time na Mery me . (kushoto ) Ni Msanii Mwanaisha Nyange (a.k.a DYANA)


Msanii Richie Mavoko (a.k.a) kulia, pamoja na Msanii Mwanaisha Nyange (kushoto) a.k.a- DYANA wakionyesha minjonjo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam wakati wakitoa shukrani kwa wadau wa muziki nchini kwaniaba ya kampuni ya  Aljazerra Entertaiment ambayo ilianza kazi zake 01-04-2004 za kuwa saidia wasanii mbalimbali wenye vipaji vya kuimba, kucheza na maagizo. Hadi sasa imefanikiwa kumtoa kisanii (kujulikana na mafanikio) Diamond Plutim, Sam wa Ukweli, Dyana, na Richie Mavoko na wengine wengi,

Msanii wa kike anaechipukia na kung”ara katika fani ya muziki nchini Tanzania, Mwanaisha Nyange (a.k.a- Dyana) akiongea na waandishi wa habari (hawapo) pichani Dec, 28,2012 jijini Dar es Salaam , ametoa shukranii zake  kwa Aljazerra Entertaiment kwa kumsaidia kumtoa msanii huyo kimuziki , bila ya kuwasahau,   wadau  mbalimbali wote wa muziki nchini ambao amesema  ndio waliomsaidia kumfikisha hapo alipo sasa katika sanaa hii ya muziki huu  wa kizazi kipya , kwani bila ya kupata ushirikiano wao asingeweza kufikia hapa alipo. . (kushoto) ni Msemaji wa  Aljazerra  Entertaiment  Simon John .. 


Previous Post Next Post