KAMPUNI YA REX ENERGY YATOA MSAADA WA CHAKULA KWA YATIMA



wafanyakazi wa Rex Energy wakiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi wa vituo vinne vya kulelea watoto vya Msimbazi Center Children Home, Buguruni Viziwi, Uhuru Mchanganyiko na Tanzania Mitindo House nje ya kituo cha Msimbazi Center.
wafanyakazi wa Rex Energy (toka kulia) Diana Mokiwa, Medard Rweikiza, Vera Bosco na Meneja wao Vincent Mughwai wakiwa na watoto yatima wa kituo cha Msimbazi Center Children Home.
Vincent Mughwai na timu yake wakiwa na watoto yatima wa Msimbazi Center Children Home.
Kiongozi mkuu wa Kituo cha kulelea watoto cha Msimbazi Center Children Hom, akipoea vyakula toka Kampuni ya Rex Energy.
Mlezi wa shule ya viziwi Buguruni akitoa shukrani kwa kampuni ya Rex baada ya kupewa vyakula.
Vincent Mughwai, Meneja Uendelezaji Biashara, Rex Energy akiwashukuru walezi wa vituo hivyo na pia kutoa salamu za Christmas na mwaka mpya kwa watoto yatima kwa niaba ya kampuni yao.

Kampuni yetu ya Rex Energy, wataalamu wa Solar, tulitoa msaada wa chakula kwaajili ya Christmas na Mwaka mpya kwa watoto yatima kutoka vituo vinne vya kulelea watoto vilivyoko hapa Dar: 

Msimbazi Center Children Home, Shule ya Uhuru Mchanganyiko, Buguruni Viziwi na kituo cha watoto cha Tanzania Mitindo House kilichoko Magomeni.

Tulitoa vyakula mbali mbali ili watoto hawa waweze kusherehekea Christmas angalau kwa kupata chakula kizuri. 

Tulitoa (kwa kila kituo) gunia la mchele (kilo 100), sukari (kilo 50), mafuta ya kupikia madumu mawili (ya lita 50 na 25), pamoja na mbuzi mnono kwaajili ya kitoweo.
Previous Post Next Post

Popular Items