BALOZI PETER KALLAGHE AKUTANA NA MAOFISA WA BODI YA UTALII TTB


Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Balozi Peter Kallaghe leo ameitisha mkutano kati yake na maofisa wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) na maofisa wa Ubalozi ili kuzungumza nao na  kupata taarifa muhimu  juu ya maadandalizi ya ushiriki wa Tanzania katika maonyesho ya utalii ya dunia (WTM), yanayotarajiwa kuanza siku ya Jumatatu Novemba 5 mpaka Novemba 8 mwaka huu katika jiji la London.

Maonyesho ya Utalii ya (WTM)  yanayoandaliwa nchini Uingereza ni maonyesho makubwa  na yanashirikisha makampuni kutoka mataifa mbalimbali duniani kwa ajili ya kuuza bidhaa zao, hasa Mahoteli, Makampuni ya Ndege na makampuni ya Utalii, Mwaka huu Tanzania inashirikisha makampuni zaidi ya 55 kutoka Tanzania Bara na Visiwani.

Katika picha juu akisisitiza jambo katika mkutano huo,  ambapo aliuliza kila jambo ambalo linahitaji kupata majawabu muhimu kabla ya kuanza kwa maonyesho hayo.

Meneja Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Bw. Geofrey Meena akifafanua jambo katika mkutano huo, kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Bi. Devotha Mdachi.

 Maofisa wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) na Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza wakimsikiliza kwa makini Mh. Balozi Peter Kallaghe wakati akizungumza nao katika mkutano huo.
Balozi Peter Kallaghe akiwa katika picha ya pamoja na maofisa wa Ubalozi na Bodi ya Utalii Tanzania TTB katika ubalozi huo mara baada ya kumalizika kwa mkutano huo.
Previous Post Next Post

Popular Items