Profesa Sherrif naye alikuwa mtoa mada
Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Tanzania Bwana Deus Kibamba akitoa mada kwa waandishi wa habari iliyofanyika mjini dodoma kwa lengo la kuwajengea uwezo katika mchakato wa Katiba Mpya ya Tanzania
Baadhi Ya washiriki
Na Jr Botea --
Dodoma WAANDISHI wa habari nchini wametakiwa kuhakikisha wanaandika habari za kuwahamasisha watanzania kujitokeza kutoa maoni yao juu ya uundwaji wa katiba mpya kwani tume ya ukusanyaji maoni imeshindwa kutekeleza wajibu wao ipasavyo. Kwa mujibu wa maelezo ya Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Tanzania , Deus Kibamba wakati alipokuwa akitoa mada yake juu ya uun dwaji wa katiba mpya katika mafunzo ya waandishi wa habari kutoka mikoa yote ya Tanzania bara na Zanzibar yaliyofanyika mjini hapa. Alisema kuwa kuna kila sababu ya watanzania wengi kutoa maoni yao kwa kutaka katiba mpya kwani katiba ya sasa ina mapungufu makubwa . Alisema kuwa katika katiba ambayo inatumika kwa sasa ina vifungu ambavyo vinapingana jambo ambalo linasababisha katiba kutokuwa katika usahihi ambao unatakiwa na bilia kutoa maoni ya kuundwa kwa katiba mpya ni wazi uchafu huo utaendelea kuwepo ndani ya katiba mpya. Mbali na hilo alisema kuwa kati ya mambo ambayo yanatakiwa kutoondolewa katika katiba ni pamoja na ibala ya 18 na ibala ya 8 ambayo kwa kiasi kikubwa inavyunjwa na viongozi waliopo madarakani. Kwa maelezo zaidi ya Kibamba alidai kuwa pamoja na kuwepo kwa tume ambayo inazunguka nchi nzima kwa ajili ya kukusanya maoni ya mchakato wa katiba mpya na kupewa fedha nyingi ambazo ni bilioni 34 lakini tume hiyo imeshindwa kuwafikia watanzania wengi . Alisema inashangaza kuona tume hiyo ambayo imepewa fedha nyingi lakini inashindwa kuwafikia watanzania wengi hususani wale waliopo vijiji jambo ambalo linaonyesha dhairi kuwa wapo watanzania wengi ambao watakosa fursa ya kutoa maoni yao. Akiendelea kutoa mada kwa waandishi wa habari juu ya uundwaji wa katiba mpya alisema wabunge wabaki kama wabunge na wasiingilie katika uvunjaji wa katiba iliyopo na kuunda mpya bali wanatakiwa kuwashirikisha baadhi ya wananchi pamoja na waandishi wa habari ama wakitaka kufanya hivyo basi wanatakiwa kuacha nafasi zao walizonazo. Aidha alieleza kuwa kuna uwezekano mkubwa wa katiba mpya kutoweza kutumika mwaka 2014 kama ilivyokusudiwa kutokana na kuwepo kwa changamoto mbalimbali ambazo haziwezi kuruhusu katiba kutumika kwa muda mwafaka.

Tags:
Social