
Mwandishi mmoja wa habari maarufu wa Ugiriki ambaye alichapisha majina ya zaidi ya raia matajiri 2,000 wa Ugiriki walio na akaunti zao katika benki za Uswisi amefikisha mahakamani akikabiliwa na mashitaka ya kukiuka sheria ya faragha.
Mwandishi huyo Costos Vaxevanis (pichani kushoto) ambaye ni Mhariri wa jarida la kila wiki la “Hot Doc”, alikamatwa mwishoni mwa wiki kwa kuchapisha orodha ambayo maafisa wa Ufaransa waliikabidhi Ugiriki mnamo mwaka wa 2010, ili wenye akaunti hizo wachunguzwe kwa tuhuma za kukwepa kulipa kodi.
Orodha hiyo na jinsi ilivyopitishwa kutoka kwa Afisa mmoja hadi mwengine bila yeyote kuchukua hatua ya kisheria, imewavutia Wagiriki.
Raia wa Ugiriki wana hasira na tabaka la wanasiasa ambao wengi wanaamini kuwa hawana nia ya kuwachunguza watu matajiri nchini humo.
Vexevanis huenda akakabiliwa na kifungo cha hadi miaka miwili kama atapatikana na hatia ya mashitaka hayo.
Tags:
Uncategolized