Fainali za shindano la Redds Miss Tanzania 2012 zinatarajiwa kufanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Blue Pearl uliopo Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam Novemba 3 2012.
Akiweka wazi kwa waandishi wa habari Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino Agency Bw. Hashim Lundenga (pichani kulia) amesema kutokana na ukubwa wa shindano la mwaka huu, wale wote watakaofanikiwa kuingia ukumbini watakaa katika viti maalum vilivyowekwa katika hadhi ya kimataifa.
Aidha amewataka wadau kutarajia shindano lenye ushindani mkubwa hasa kwa kuzingatia kuwa sehemu kubwa ya warembo ni wasomi walio katika ngazi ya elimu ya juu nchini.
Mo Blog inakudokeza kuwa tiketi zinaanza kuuzwa leo hii katika vituo vilivyochaguliwa na pia katika shindano hilo Diamond Platinum, ‘Rachel’ na Wanne Star Ngoma Troupe watawasha moto wa burudani. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Kamati ya Miss Tanzania, Bw. Bosco Majaliwa.