Video: Alichozungumza T.I baada ya kuhojiwa kuhusiana na Ebola Tanzania

Rapper T.I Baada ya show Jumamosi, aliondoka Tanzania Jumapili kurudi kwao Marekani kwa ajili ya kuhakikisha mauzo yanaenda vizuri katika album yake mpya ilikua inatoka Jumanne ya October 21.


Akiwa NewYork T.I alijikuta yuko mbele ya camera akihojiwa na mwandishi wa habari aliemuuliza kuhusu ishu ya Iggy na Snoop ambayo alisaidia kuimaliza na baada ya hapo akamuuliza T.I vp Tanzania ilikuaje? Ebola je?



T.I alichojibu ni hiki “Tanzania ilikua poa sana, sijaona Ebola yoyote wala kuona hata dalili za kuwepo kwa ugonjwa huo, sijaona chochote cha kunifanya niifikirie Ebola au kuhisi uwepo wake”
Previous Post Next Post