Tyga amuita Drake ‘fake’, asema yupo Young Money sababu ya Lil Wayne

Tyga amemchana rapper mwenzie wa Young Money, Drake kuwa ni fake.Mapema mwezi huu, rapper huyo alidai kuwa Young Money imemshikilia matekana na kutishia kujiondoa kama hawatampa tarehe ya kuachia album yake ya ‘The Gold Album: 18th Dynasty.

Baada ya tweets zake, rais wa Young Money Mack Maine alijibu mapigo huku Nicki Minaj akimunfollow kwenye Twitter. Akiongea na jarida la VIBE, Tyga amesema:




“Nataka kujitegemea. Sipatani na Drake. Sipatani na Nicki. Simpendi Drake kama mtu. Ni feki kwangu. Napenda muziki wake lakini sisi ni watu tofauti. Tulilazimishwa kuwa pamoja na ni kama tulikuwa tunalazimisha uhusiano. Lil Wayne alikuwa gundi iliyoshikilia uhusiano. 

Mwisho wa siku sababu ya kusaini na Young Money ni sababu ya Wayne. Sio sababu ya Drake, sio sababu ua Nicki. Ilikuwa ni sababu ya Wayne na uhusiano wangu naye,” alisema.

“Najaribu kuwa mtu mzuri kwa kila mmoja, lakini wakati mwingine kila mtu ana tabia, malengo na hulka tofauti. Ukigundua hilo, utagundua kuwa hiyo sehemu ambayo unataka kuendelea kukua.”

Tyga amesema rafiki yake mkubwa ni Chris Brown. “Huyo ndio rafiki yangu halisi. Tunakuwa pamoja muda wote.”

Rapper huyo ataungana na Chris na Trey Songz kwenye ziara yao ya pamoja na pia kufanya album nyingine pamoja, ‘Fan of a Fan 2’.
Previous Post Next Post