Diamond : “Baba yangu alikua miongoni mwa matajiri wa Tanzania” , stori nzima iko hapa…

Katika interview yake aliyoifanya na kipindi cha Sporah Show , Diamond Platnumz ameongelea vitu vingi sana ambavyo ni mara ya kwanza kuwahi kuvisema. Sporah alimuuliza Diamond Swali hili “Je, unamsaidiaga baba yako , kwa mfano kama kuna kitu chochote anataka au kuna kitu hakipo sawa ? ” , Diamond alimjibu hivi , “Sio kivile.Unajua alikua ni mmoja wa watu matajiri Tanzania, kwahiyo sijui kama bado ana pesa au hana, lakini kama hakina na akiniambia anataka kitu nitampa , lakini siwezi kwenda na kumuuliza kama anataka kitu, lakini naweza kumuuliza mama yangu”



Sporah pia alimuuliza Diamond kama baba yake aliyomkataa kwenye umri mdogo alimrudia pale aliposikia Diamond ametoka kimuziki na Diamond alifunguka hivi , “Yes, alinirudia, na mimi nilimwambia siwezi kukuchukia baba lakini sitakua na mapenzi ambayo mtoto inabidi awe nayo kwa baba yake , lakini yeye bado ni baba yangu , ataendelea kua baba yangu lakini ikija kwa mama yangu , ni mama yangu , huwezi kumlinganisha mama yangu na baba yangu,ni tofauti,tofauti kabisa ” .




Sporah aliendelea na kumuliza Diamond ni mahusiano gani hasa anayo kwa baba yake . “Ni ya kawaida. Na kaa na mama yangu,siwezi kukaa muda bila kuwasiliana na mama yangu lakini naweza kukaa mwezi bila kuwasiliana na baba yangu , najaribu maranyingine lakini ni vigumu na siwezi sababu sijazoea” Full interview hii hapa..
Previous Post Next Post

Popular Items