Tigo Pesa kugawa faida kwa wateja Tanzania

Kampuni ya Tigo nchini Tanzania imetangaza kuwa itasambaza kiasi cha shilingi bilioni 14.25 (dola mil. 8.7) kama faida walioipata kwenye Akaunti ya Mfuko wa Tigo Pesa, kwa mamilioni ya wateja wake, na kuwa kampuni ya kwanza ya simu za mkononi duniani kutoa faida ya Mfuko wa Akaunti yake, kupitia pesa za simu.

Mfuko wa Tigo Pesa ni akaunti ambayo fedha zote kutoka kwa watumiaji wa Tigo Pesa zimekuwa zikiwekwa tangu kuanzishwa kwa huduma hiyo miaka miaka minne iliyopita. Kwa sasa Tigo wako katika nafasi ya kuweza kugawanya faida hizo kufuatia kibali kutoka Benki Kuu ya Tanzania kwenye barua ya kukubaliwa ya mwezi Julai.



Meneja Mkuu wa Tigo Diego Guiterrez alisema kwamba kiasi cha faida hiyo kitawafunaisha washika dau wote wa Tigo Pesa, wakiwemo mawakala wa jumla, mawakala wa rejareja, na wateja kwa ujumla.

“Kwa miaka mitatu na nusu iliyopita Mfuko wa Tigo Pesa umekuwa ukikusanya marejesho ya kiasi cha asilimia 5 na 12 ambacho kimefikia shilingi bilioni 14.25 mwezi Juni mwaka huu. Lengo la kugawanya fedha hizi ni kutoa fursa kwa washika dau wote wa Tigo Pesa, marejesho kupata kile walichowekeza kulingana na kiasi cha pesa kwa mfumo wa mtandao walichoweka kwenye mfuko wao wa Tigo Pesa,” alisema Guiterrez..

Aliongeza: “Wastani wa marejesho ambao washika dau watakayopokea utatofautiana kulingana na wastani wa pesa wanazoweka kwenye mifuko yao mitandao ya Tigo Pesa kila siku, awe ni wakala mkuu, wakala wa rejareja au mteja.”

Tigo wanatarajia kwamba mgawanyo huo utawanufaisha watumiaji milioni 3.5 wa Tigo Pesa nchini, wakiwemo mawakala wakuu na warejareja ambao ni sehemu ya muunganiko wa huduma ya mtandao wa pesa nchini Tanzania.
Previous Post Next Post