Kanye West alazwa hospitali nchini Australia baada ya kuugua gafla kabla ya shoo

Kanye West alipelekwa na kulazwa kwenye hospitali nchini Australia na kufanyiwa scan ya ubongo wake kutokana maumivu makali ya kichwa.





Staa huyo alikuwa apande jukwaani kutumbuiza huko Melbourne jioni ya September 10 kabla hajaugua ghafla mida ya saa nane mchana. Mwanamke mmoja aitwaye Loraine Kelly, ambaye mwanae alikuwa amelazwa kwenye hospitali ya Epworth ya Richmond ameliambia jarida la Women’s Day kuwa Kanye na mke wake Kim Kardashian West na wapambe wao waliingia hospitalini hapo kupitia mlango wa nyuma akiwa amejifunika uso wake kujificha.

Anasema staa huyo aliwekwa kwenye kitanda cha kubebea wagonjwa kabla ya kupelewa kwenye chumba cha MRI.

E! Online imeripoti kuwa Kanye na Kim waliondoka kwenye hospitali hiyo saa 10 na nusu jioni na kurejea kwenye hoteli waliyokuwa wamefikia.
Previous Post Next Post

Popular Items

EXPENSIVE THING OF THE DAY

New Music: Blue - Pesa