Jux afunguka tetesi za kuhusu wimbo wake mpya ‘Sisikii’ kama amemuimbia Vanessa Mdee

Mwimbaji wa R&B Jux ameendelea kukana tetesi za kuwa na uhusiano na Vanessa Mdee aka Vee money , ambao wameonekana kuwa karibu sana kwa siku za karibuni. Tetesi hizo zimepelekea watu kuhisi kuwa wimbo wake mpya ‘Sisikii’ alioutoa wiki hii amemuimbia Vanessa.





Hii si mara ya kwanza kwa Jux kusemekana kutoa wimbo ambao amemwimbia msichana, baada ya kutoa single yake iliyopita ‘Nitasubiri’ ambayo ilisemekana alimwimbia Jacky Cliff, na sasa wimbo wake mpya ‘Sisikii’ inadaiwa kuwa amemwimbia Vee Money.

Hili ndio jibu la Jux kuhusu ukweli wa kama amemwimbia mwimbaji wa ‘Closer’ kupitia XXL ya Clouds Fm.

“Watu wanasema umemwimbia flani na Sio mara moja nimeshaskia hata wakati naimba ‘Uzuri wako’, nimemwimbia nani…mimi niko tofauti naweza nikasema hivyo kwasababu sijawahi kwenye maisha yangu kusema hata siku moja nikishika pen nimemwandikia msichana wimbo, na sijawahi kwenye nyimbo yangu hata moja kutamka jina lolote la mwanamke nyimbo zangu zote…Kwahiyo hii nyimbo ya ‘Sisikii’ inawezekana labda kwa story ambazo zinasemwa na mambo yanayoskika wakajumlisha watu vituu.”



Previous Post Next Post