Huyu ndiye Pastor anayetuhumiwa kuisaliti ndoa yake kwa kuzini na mwanamke mwingine

Mwanzilishi wa kanisa la Christ Embassy na mhubiri maarufu, Pastor Christian Oyakhilome anatuhumiwa kusaliti ndoa yake na sasa mke wake Rev. Anita Odegwa Oyakhilome amedai talaka



Mke wake anadai talaka yake kwa kile alichokidai kuwa ni sababu ya ‘tabia mbaya’ na ‘uzinifu’. Jitihada za kuwapatanisha wawili hao ambao kanisa lao ni miongoni mwa makanisa maarufu nchini Nigeria na lenye matawi duniani kote (ikiwemo Tanzania) zimegonga mwamba.



Wana watoto wawili wa kike, Sharon na Charlyn.


Mchungaji huyo kwa mujibu wa wazee wa kanisa amekanusha madai ya kuzini na anaamini kuwa mke wake ameshawishiwa na marafiki wabaya wenye lengo la kuvuruga ndoa yao.

Chris pia anamtuhumu mkewe kwa kutaka kumpindua.

Previous Post Next Post