Hii ndio orodha ya waigizaji 10 wa runinga waliolipwa pesa nyingi zaidi 2014

Sofia Vergara ameongoza orodha ya majina kumi ya waigizaji wa vipindi vya runinga waliolipwa pesa nyingi mwaka 2014.

Muigizaji huyo mwenye umri wa miaka 42 ameingiza kiasi cha $37 million (sawa na 61,549,500,000 za Tanzania), ikiwa ni ongozeko la $ 7 Million alizoingiza mwaka jana.



Hii inamfanya kukaa kwenye kilele cha orodha hiyo kwa mwaka wa tatu huku pesa nyingi zaidi ikiingia kupitia endorsements.

Sofia Vergara ni muigizaji wa Colombia, mchekeshaji, mtangazaji wa vipindi vya TV na mwanamitindo pia. Alipata umaarufu zaidi awali miaka ya 1990 alipokuwa mtangazaji wa vipindi viwili vya television vinavyotumia lugha ya kihispania.

Hii ndio orodha kamili:

2.Mariska Hargitay(Law & Order)- $13 million.

3. Kaley Cuoco-Sweeting – (The Big Bang Theory)-$11 million.

4. Julianna Margulies, Ellen Pompeo and Cobie Smulders – $10 million.

5. Alyson Hannigan , $9.5 million

6: Amy Poehler (Parks & Recreation)-$7 million

7: Mindy Kaling (The Mindy Project)-$6.5 million

8 (TIE): Kerry Washington ,Zooey Deschanel,Courteney Cox-$6 million

9.Claire Danes ( My So-Called Life)-$5 million

10: Lena Dunham-(Girls)-$3.5 million
Previous Post Next Post