Wanasiasa wakubwa wanaonifuata kipindi chauchaguzi waweke wazi 'Manyaunyau' aelezea anavyowafanyia

Mganga maarufu wa jadi  anaefahamika kama Dr. Manyaunyau amesema kinapofika kipindi cha uchaguzi, wanasiasa wengi wakubwa humfuata kwa lengo la kutaka awasaidie lakini siku zote wanafanya kwa kujificha sana.


Manyaunyau amewataka wanasiasa hao kutofanya kwa siri kwa kuwa anachokifanya yeye ni ufundi wa jadi ambao nchi nyingine unajulikana mwanasiasa huweka wazi benchi lake la ufundi kwa kujigamba.

“Viongozi kwa kweli wanatufuata inapofika wakati wa uchaguzi. Si unajua wasiwasi, wanasema wasiwasi ndio akili. Kwa hiyo wanakuja lakini katika njia ya kuangalia. Mambo hayo hapa Tanzania ndio watu wanayaona mageni kiongozi kwenda kwa mganga wa kienyeji, wengine wanakuja kwa kujificha. Na mimi nawaambia ‘kwanini unajificha na wewe ni binadamu?’ Lakini nchi nyingine za Kiafrika unakuta President ana mganga wake kabisa. ‘Huyu ni kamati yangu ufundi’ anakwambia.” Ameesema Manyaunyau.

“Sasa watu wanashindwa kutuchukua sisi kutuweka Live kamati ya ufundi matokeo yake wanajificha ndio unawapa maneno wakibahatisha kukujua. Kuwa tu free ‘ebana mimi nina Dr Manyaunyau ndio kamati yangu ya ufundi. Husikii mtu akiongea. Ila ukijifichaficha ndio unakipaisha kitu…” Ameongeza.


Akielezea kile anachokifanya hasa wakati wa uchaguzi ili kumsaidia mgombea. Manyaunyau amesema wanaweza kumsaidia mgombea aliyepungukiwa wafuasi kupata wafuasi wapya kutoka kwa mwenzake.

“Inasaidia, lazima kete wakati mwingine uzicheze kidogo. Akili za watu lazima ucheze nazo pale. Kwa hiyo wakati mwingine…si unajua bana mbona wako wengi na huku kwangu wamekuwa hivi?’ ‘Basi ngoja tumpunguzie tukuwekee na wewe… ndio shughuli zetu hizo na inakuwa.”

Mganga huyo anaeleza kuwa wapo wanasiasa wengi waliomfuata ameweza kuwasaidia na wakafanikiwa kuzikusanya kura za wananchi.

“Wengi..wengine hatuwezi kuwataja majina yao. Lakini wengi tumewapeleka mjengoni kule. Serious nakwambia, lakini hizo ni taratibu zetu ambazo zipo.” Ameeleza.

Hata hivyo suala la imani kama hii ni tata sana katika jamii na hakuna anaeweza kuthibisha kuhusu nguvu hiyo ya ushindi katika uchaguzi na ibaki kuwa ‘unaamini au hauamini’!

Ni sera bora au kuna nyongeza katika sanaa ya siasa? Kila mtu ana jibu lake.

credt:tmsfm
Previous Post Next Post