Picha: Jaguar atoa majibu ya picha zake akiwa na mrembo kanisani wakifunga ndoa

Katika wiki iliyopita Hit maker wa ‘Kioo’, na anayetamba na wimbo wake mpya wa One Centimeter Jaguar kutoka Kenya alitawala vichwa vingi vya habari nchini Kenya baada ya baadhi ya picha zake zikimuonesha yuko kanisani akitimiza moja ya hatua muhimu katika maisha ya mwanadamu (ndoa).


 Baadhi ya vichwa vya habari hiyo vilisomeka ‘Jaguar holds secret wedding in South Africa?’, ‘Jaguar weds in South Africa’.



Hata hivyo Jaguar ameweka wazi ukweli wa picha hizo kuwa ni video yake mpya:
“…….a pic from my upcoming video 0ne centimetre droppin 2morrow”, aliandika Instagram.

Jaguar ameachia single mpya iitwayo ‘Centimeter’ ambayo video yake inatarajiwa kutoka leo Jumatatu (Agosti 25)

“…..Get ready for one centimeter video today…..#next level”.

Previous Post Next Post