Sasa ni zamu ya Shaa kwenye Coke Studio Africa, baada ya Vee Money na Joh Makini

Mwaka huu Coke Studio Africa imeamua kuchukua wasanii wengi zaidi nchini kushiriki kwenye kipindi hicho, na sasa ni zamu ya mwanadada Shaa baada ya Vee Money na Joh Makini.



Shaa akiwa na Jackie

Baada ya Vanessa Mdee kuungana na msanii wa Nigeria, Burna Boy na Joh Makini kurekodi na Chidinma wa Nigeria, sasa ni zamu ya Shaa ambaye yupo Nairobi, Kenya kurekodi kwenye kipindi hicho na msanii wa Uganda, Jackie Chandiru.

“Ndani ya #CokeStudioAfrica wiki hii Malkia wa Uswazi nikiwa na @JackieChandiru #WanawakeOyeeee hahahah,” ameandika Shaa kwenye Twitter.


Previous Post Next Post