Shilole afunguka kuhusu Nuh Mziwanda kujichora tattoo yenye jina lake ‘Ni mapenzi tu na Mimi nikiamua Nitachora’

 Baada ya Nuh Mziwanda kuamua kuchora tattoo isiyofutika ya jina la malkia wake wa moyo Shilole aka ShiShi Baby, masbabiki wengi walitoa mitazamo yao tofauti kuhusina ana uamuzi huu wa Nuh Mziwanda kujichora tattoo zisizofutika ,Lakini tukiachana na Mashabiki Je Shilole Mwenye anasemaje kuhusiana na hili..!


Nuh Mziwanda akiwa na Shilole Kimahaba zaidi

Akizungumzia uamuzi wa mpenzi wake, Shilole amesema huo ni uamuzi mgumu sana aliouchukua na amefurahishwa sana na uamuzi huo.




“Hata sijui nisemeje…unajua kuchora kitu kwenye mwili ambacho sio cha kwako ni ngumu sana. Kwa hiyo yeye uamuzi wake aliouchukua, hakulazimishwa na mtu alifanya mwenyewe kwa mapenzi. Kwa hiyo aliamua kwa kuwa analove na mimi na ninalove na yeye basi ndio maana akaamua kufanya vile. Mimi kwangu ina maana kubwa sana sio siri ambayo haielezeki.”

Shilole alizungumzia pia mpango wa kulipa wema wa Mziwanda kama nay eye atachora tattoo ya jina la Mziwanda au la!
Tatoo alizochora Nuh Mziwanda zenye jina la Shilole
“Hamna…siwezi kusema ntafanya hivyo sijui na nini basi ni mapenzi tu na mimi siku nikiamua kufanya ntafanya kama ambavyo amefanya yeye. Kiukweli ana love ya ukweli kabisa tofauti na wanaume ambao nilikuwa nao, watu walikuwa wanapenda tu wasikie wanatoka na ShiShi kwa kutaka kutafuta ‘kick’ na nini…lakini Nu h kama Nuh ana upendo wa peke yake kabisa. Yaani hadi inafikia hatua nasema alikuwa wapi. Wanasema Mungu akitaka kukupa kitu hakuandikii barua.”
Previous Post Next Post

Popular Items

EXPENSIVE THING OF THE DAY

New Music: Blue - Pesa