Kombe la Dunia: Uholanzi yaifunga Hispania mabao 5-1, Van Persie na Robben wang’ara

Mabingwa watetezi wa kombe la dunia, Hispania wamerudishwa darasani na Waholanzi waliokuwa na hasira ya kulipiza kisasi cha kufungwa kwenye fainali ya mwaka 2010 kwa kupokea kichapo cha aibu cha mabao matano kwa moja.


Katika fainali ya mwaka 2010, Andres Iniesta alifunga goli katika dakika za nyongeza na kuifanya ishinde bao 1-0 na kuchukua kombe la dunia nchini Afrika Kusini. Bao la kwanza na la pekee la Hispania lilifungwa na Xabi Alonso katika dakika ya 27 kupitia penalty.

Robin Van Persie alisawazisha goli dakika 44 ya kipindi cha kwanza kwa kichwa cha kupaa angani kilichowagusa wengi.


Dakika ya 53 Arjen Robben alipachika bao la 2, kabla ya Stefan de Vrij kuweka jingine katika dakika ya 64. Van Persie aliongeza la nne katika dakika ya 72 kabla ya Robben kupiga msumari wa mwisho dakika ya 80 na kufanya mabao yawe 5-1.

Previous Post Next Post