Hemedy PHD mpenzi wa filamu

Msanii wa Filamu na Muziki hapa Bongo, Hemedy PHD ameweka wazi kuwa, katika mambo ambayo anapenda kufanya wakati akiwa nje ya kazi ni kwenda Cinema kutazama filamu.

Muigizaji na mwimbaji Hemedy PHD

Hemedy amesema hii ni nafasi ambayo inamuwezesha kukutana pia na watu wa daraja fulani la juu la maisha ambao mara nyingi huzungumza na kubadilishana mawazo.

Hemedy ambaye kwa sasa ameachia video yake mpya ya My Weding Day, amesema kuwa, anafarijika sana anapokutana na watu wa aina hii ambao wanakuwa wanaelewa kazi zake, huku akikiri ukweli kuwa watu hawa huwa si wapenzi wa muziki na filamu za bongo.
Previous Post Next Post