‘The National Church of Bey’ Ni kanisa Jipya liloanzishwa na Mashabiki wa Beyonce Marekani

Kutokana na kuvutia mashabiki wengi Duniani kote na kuwa na kuwa na mashabiki wengi Dunaiani kote mama wa Blue ivy a.k.a Beyonce "King Bey" kirefu chake ni KING BEYOND kama anavyojiita mwenyewe , mashabiki wake hao waishio marekani wameamua kuanzisha linalo mtukuza Beyonce


Kanisa hilo limepewa jina “The National Church of Bey” na limeanzishwa na kundi la marafiki ambao hukusanyika kila Jumapili kuimba nyimbo za Beyonce kutukuza dini iitwayo ‘Beyism’ ambayo inahusiana na Beyonce. Mwanzilishi wa kanisa hilo, Pauline John Andrews amesema anafedheheshwa na jinsi umma unavyoshindwa kutambua uwepo wa mtu mtakatifu kama Beyonce.
Kwa mujibu wa taarifa, kanisa hilo limechapisha hadi biblia ‘Beyble’ na itaanza kupatikana mtaani bure hivi karibuni. Kundi hilo linatarajia kujenga kanisa lake na litajitanua zaidi hadi nje ya Atlanta, lililokoanzia.
Kanisa likikamilia, wamepanga kumwalika staa huyo ili azungumze.

Previous Post Next Post

Popular Items

WAKUU WA USALAMA KUHOJIWA KENYA