Picha: H.Baba amkumbuka James Dandu 'Mtoto wa Dandu" kwa kutembelea kaburi lake Mwanza

H.Baba ambaye ni msabaye ni msanii wa muziki hivi karibuni alilitembelea kaburi la mmoja wa waasisi wa tuzo za muziki za Tanzania, KTMA na msanii wa muziki marehemu James Dandu aka Cool James.



Kupitia Instagram H.Baba ameandika: Nipo Ngudu Kwimba apo ndipo alipopumzishwa shujaa wetu wa mwanza Cool James Dandu, Nilienda kusafisha kabuli lake nakushirikiana na ndugu zake kiukweli nilipokelewa vizuri sana nyumbani kwao nafamilia ya Dandu nikamuona na mzee Dandu mwenyewe . Wasanii wenzangu muwe mnapita japo kwa shujaa wetu,kuna leo na kesho nawewe haupo wasanii wenzio watakupotezea ata kama umetenda mema kiasi gani? Jitambue kijana nimuda wako ila kumbuka kunakufa pia, tukumbuke kusali nakumuomba mungu tunapokwenda atupajui?”Alisema H.Baba

H.Baba akifanya usafi kwenye kaburi la Dandu

H.Baba akiwa kwenye kaburi la marehemu Dandu na baadhi ya ndugu wa Dandu

H.Baba akiwa na wazazi wa marehemu Dandu
Katika picha nyingine msanii huyo aliandika: Nawaasa wasanii wenzangu mnaoshiriki tuzo za Kill Music Awards mkibahatika kupata tuzo hii yenye heshima kubwa Tanzania ipelekeni kwa mtoto wa Dandu atafurahi sana japo katutangulia mbele za haki,nawaombea kwa Watanzania wote wawapigie kura wanamuziki wa mwanza kwenye Kill ili tupeleke tuzo kwa ndugu yetu kaka yetu mwanamuziki mwenzetu alieitangaza Tanzania kimuziki Kimataifa nakitaifa .. Mungu ibariki mza tufanikishe hili #mpigie kura @fidQ @youngkillermsodoki ili tufikishe ushindi wetu pale kwa familia ya dandu . #kwimba ngudu. Tunakaribisha ata kama msaanii mwingine akijitolea kama msanii Kala Jeremah alivyofanya mwaka jana kwakupeleka tuzo kwa mama yake na Mangwea, r.i.p Dandu, r.i.p Sharobalo, r.i.p Langa, r.i.p Mr.Ebbo, r.i.p Stive2k, r.i.p Complex r.i.p Lady Luu r.i.p N.K … Sote tupo njia moja tujiandae.”


Previous Post Next Post