Hawa ndio wasanii 6 wa kike wa bongo fleva wenye mvuto zaidi.

Leo katika safu yetu ya 'FACT WITH BONGO61' tunakuletea walimbwende 6 wa Bongoflava wenye mvuto zaidi hii ni kwa upande wa Bongo61.Com. machaguo haya ya wasanii 6 wa kike wenye mvuto Bongo yamefanywa na Bongo61 na sio kwa kumpigia mtu kura.



Hawa ndio wasanii wa kike wenye mvuto zaidi katika tasnia ya muziki wa Bongo Flava

Vanessa Mdee.


Maarufu kama Vee money  yeye ni recording artist, rapper, songwriter, na mtangazaji wa vipindi vya television na redio,mitandao mengi ya huko nchini Kenya ili ripotiwa kumfananisha mrembo huyu na mmoja wa wanamuziki wa destiny child,Kelly Rowland.ndiye msanii anayetoka poa kwenye kila aina ya vazi atakaloamua atupie,unaweza kudhani kuwa ni model au kwa nini hajawa model nakuchagua kuwa muimbaji kwa jinsi alivyo tu.
Najma.

Sauti yake na uzuri wake kwa mara ya kwanza kuonekana katika luninga,ni kwenye video ya tabasamu ya Mr.Blue,ila kutokana na uzuri wake,naamini asilimia kubwa ya watu huishia kumuangalia Najma tu,naamini hata asingekuwa na sauti nzuri watu bado wangekuwa wanaangalia video zake,mbali na uzuri huo yeye pia ni msanii wa bongo fleva na kwa hivi sasa ana-hit na track yake mpya ya Nimechoka aliyomshirikisha Aslay.
Meninah
Urembo wake ulijionyesha pamoja na kipaji chake kizuri cha kuimba pale alipoamua kushiriki mashindano ya Epic Bongo Star Search,ndio Tanzania ilipoanza kuona uwepo wake,Shaghala baghala ndiye video yake iliyomuweka kwenye ramani ya bongo fleva mwaka huu,nakufanikiwa kuzidi kupata umaarufu,uzuri wake unaweza kusema labda amechovya flani hivi.
Jokate.
Ingawa aliweza kuonekana kwenye nyimbo kadhaa za bongo fleva hapo mwanzo, kupitia uzuri wake akiwa kama model,mwisho wa siku akajaribu kuweka vocal,zikakubalika,nakushirikishwa kwenye nyimbo mbali mbali ikiwemo kaka dada.Huyu si tu msanii wa bongo fleva,bali ni Tv presenter na host katika events mbalimbali,ukiachia mbali u-CEO of Kidoti Lovig co.
Recho.
Wengi humfananisha msanii huyu na mkongwe wa muziki wa Bongo fleva maarufu kama RayC,kuanzia macho,weupe wake,sauti hadi jinsi anavyocheza unaweza kusema kuwa ni mdogo wake Ray C,ila uzuri wake ndio uitakaokuweka kwenye luninga yako muda mrefu kumwangalia video yake,badala yakusikiliza nyimbo.Ni msanii aliyekuja kwa kasi kwenye Bongo Fleva nakukubalika kirahisi na kubaki on top hadi hii leo,ana-hit na nyimbo kama Kizunguzungu,upepo,nashukuru umerudi na nyingine nyingi.
Linah.
Ukiongelea wenye mvuto kwenye sanaa hii ya Bongo fleva,Linah anaweza kuwa juu ya list,jina lake kamili ni Linah Sanga,anakimbiza sana katika anga hizi za bongo fleva, kwenye upande mzima wa mvuto,wadau wanasema kuwa hawezi kulinganishwa na msanii mwingine yeyote.
Previous Post Next Post