Haya ndio majina ya wanaowania Tuzo za KTMA 2014

Baraza la sanaa la Taifa (BASATA)Leo limetangaza rasmi matokeo ya mchakato mzima wa kuwapata wateule rasmi wa vipengele 34 vya Tuzo za muziki Tanzania.Akiongea na waandishi wa habari Kaimu Katibu Mtendaji wa BASATA,Godfrey .L.Mngeleza alisema , zaidi ya mapendekezo 30,000 yalitumwa kwa njia ya sms na mtandaoni.



Hata hivyo alidai kuwa nyimbo ‘Uzuri wako’ ya jux,’nimevurugwa’ ya Snura na ‘tema mate tuwachape’ ya Madee zimeondolewa katika mchakato huo kwa madai kuwa zimevunja maadili na hazifai kwa jamii ya Tanzania.




Nyingine ni
WIMBO BORA WA AFRIKA MASHARIKI – Tubonge ya Jose Chameleone, Nakupenda pia ya Wyre na Alaine, Badilisha ya Jose Chameleone, Kipepeo ya Jaguar, Kiboko changu ya Amani, Weasal na Radio.
WIMBO BORA WA TAARAB – Wasiwasi wako wa Mzee Yusufu, asie kujua hakuthamini Isha na Saida Ramadhani, Nipe stara Rahima Machupa, sitaki shari Leila Rashid, fahari ya mwanamke ya Khadija Kopa, mambo bado Khadija Yusufu, kila muomba Mungu ya Mwanahawa Ally.
WIMBO BORA WA RAGGA/DANCEHALL – Nishai ya Chibwa ft Juru, Sexy Lady ya Dr. Jahson, My sweet ya Jettyman Dizano, feel alright ya Lucky Stone na wine ya Princess Delyla.
WIMBO BORA WA KUSHIRIKISHWA/KUSHIRIKIANA – Muziki gani ya Ney wa Mitego ft Diamond, Joto hasira ya Lady Jaydee ft Prof J, kidela ya Ally Kiba na Abdu Kiba, bila kukunja goti ya MwanaFA, Ay ft J Martins na tupogo ya Ommy Dimpoz ft J Martins.
RAPA BORA WA MWAKA WA BENDI – Kitokololo, Chokoraa, Ferguson, Canal Top na Totoo ze bingwa.
MTUMBUIZAJI BORA WA KIKE WA MUZIKI – Khadija kopa, Vanessa Mdee, Isha Ramadhani, Luiza Mbutu, Catherine (Cindy)
MTAYARISHAJI BORA WA NYIMBO WA MWAKA TAARAB – Enrico, Ababuu mwana wa Zanzibar na Bakunde.
MTAYARISHAJI BORA WA NYIMBO WA MWAKA (BENDI) – Allan Mapigo, C9, Enrico, Amoroso na Ababuu mwana wa Zanzibar.
WIMBO BORA WA REGGAE – Niwe nawe ya Dabo, hakuna matata ya Lonka, tell me ya Dj Aron ft Fidempha, bado nahitaji ya Chikaka ft Bless P & Lazzy B, Bongo reggae ya Warriors from the east.
WIMBO BORA WENYE VIONJO VYA ASILI YA KITANZANIA – Kwejaga nyangisha ya Batarokota, Nalonji ya Kumpeneka, bora mchawi Dar bongo massive, tumbo lamsokota ya Ashimba, Aliponji ya Wanakijiji na Agwemwana ya Cocodo african music band.

Credit : Millard Ayo
Previous Post Next Post

Popular Items