Audio: Roma Mkatoliki aeleza maana ya mistari ya 'KKK' inayomtaja Songa na Jide 'leo Jide anamjua Songa!'

Wimbo wa Roma KKK (Karibu Kwenye Karamu) uliotoka rasmi March 10 mwaka huu umeendeleza sifa za nyimbo za rapper huyo kuwa na ‘mashairi tata’.

Moja kati ya mistari hiyo ni mistari inayomtaja Lady Jay Dee kwa jina la ‘Jide’ na rapper wa Tamaduni music ‘Songa’, mistari ambayo ilikosolewa na P The MC wiki iliyopita kwa madai kuwa haiwezekani Roma ashangae Jide kumjua Songa wakati yeye pia ameanza muziki miaka aliyoanza Songa na bado Jide anamjua (Roma) na hakuna anayeshangaa.





Roma Mkatoliki ameifafanua mistari hiyo wakati anafanya mahojiano na Jabir Saleh aka Kuvichaka na One B aka Moko Biashara katika kipindi cha Bongo Dot Home ya 100.5 Times Fm.

“Hiyo mistari miwili, ‘wanatugawa kimakundi watumeze ona Anaconda...leo Jide anamjua Songa’. Game yetu inakuwa inashikiliwa na wadau, wadau wanakuwa wana-run game yetu, inakuwa kama formula.” Amesema Roma.



“Verse ya pili nimeongea kuhusu umoja wa wasanii, ili uweze kuwatawala watu wale watu wakiwa kwa pamoja, wakiwa na nguvu moja wana kauli moja na lugha moja kuwatawala ni ngumu sana. Ila wakiwa vipande vipande ni rahisi sana. Sasa game yetu imetengenezewa mazingira hayo ikawa ina matabaka. Halafu mifano mingi sana ipo ambayo tumeweza kuishuhudia kwamba kuna matabaka kati ya wasanii hawa na hawa.” Ameongeza.



Ameeleza kuwa kunapokuwa na matabaka kati ya wasanii inakuwa rahisi kutawaliwa na kwamba kuna watu ambao wanawagawa wasanii katika makundi mbalimbali ili iwe rahisi kuwatawala.

Rapper huyu akaweka msisitizo kwenye maana ya kuonesha mshangao baada ya Jide kumjua Songa wa Tamaduni Music.

“Ni kwamba tungekuwa wote tuko pamoja watu wote 100 ingekuwa ni ngumu sana mimi kukujua One B. Lakini kwa sababu tumetengenezewa mazingira tukagawa vipande kwamba ninyi wa huku na ninyi wa huku. Kile kitendo cha kutengwa ikafanikiwa kwamba aaah leo sasa One B anajuana na Roma, sasa leo Jide anajuana na Songa kwa sababu wote inabidi waongee kauli moja.” Ameeleza Roma.

Roma ameeleza kuwa pasingekuwa na tatizo kati ya wasanii na kungekuwa na umoja wasanii basi kungekuwa na umoja na ingekuwa vigumu kufahamiana mmoja mmoja.

Kipindi cha Bongo Dot Home kinakuwa hewani kila Jumamosi saa kumi kamili hadi saa moja kamili jioni.

Unaweza kusikiliza kwa kubofya sehemu iliyoandikwa ‘Listen’.



Crdit:Timesfm
Previous Post Next Post