Kuelekea kesi ya Ezibeth Michael 'Lulu' , Yajue haya

Uhusiano wa kimapenzi baina ya msanii wa filamu nchini Elizabeth Michael ‘Lulu’ anayedaiwa kumuua bila kukusudia msanii mwenzake, Marehemu Steven Kanumba, utaanza kukumbushwa tena hivi karibuni pale Lulu atakaporudishwa katika Mahakakama Kuu Tanzania Kanda ya Dar es Salaam Februari 17 mwaka huu.Lakini kabla kesi haijaanza kusikilizwa kuna mambo ya muhimu inabidi uyajue ;-



-Lulu alizaliwa mwaka 1994 elimu ya Kidato cha Nne alihitimu katika Shule ya Sekondari ya Midway, baada ya hapo aliendelea na shughuli za sanaa ambazo alizianza tangu mwaka 2000. Lulu alifahamiana na Kanumba kwa muda wa miaka 10 wakifanya kazi za sanaa na Januari mwaka 2013 ndipo walipoanza rasmi uhusiano ya kimapenzi.



katika uhusiano huo hawakuwahi kuishi pamoja isipokuwa alikuwa akienda kwa Kanumba anapojisikia na mara kadhaa aliwahi kulala huko.

kipindi cha miezi minne ya uhusiano wao, walikuwa wakigombana mara chache lakini sababu kubwa ilikuwa ni wivu wa mapenzi kwa sababu wote walikuwa hawaaminiani.


Siku ya tukio ilikuaje ? jioni ya siku hiyo Lulu alimpigia simu Kanumba na baada ya muda mfupi alikwenda nyumbani kwake Sinza Vatican.alipofika kwa Kanumba, alimkuta akiwa chumbani kwake akinywa pombe ambayo ilikuwa imechanganywa na soda na ghafla simu yake iliita na alipotoka nje kutaka kwenda kuisikiliza Kanumba alimfukuza hadi barabarani. baada ya kumpiga kwa ubapa ghafla alitupa panga chini huku akiwa amesimama alianza kupumua kwa taabu na baada ya muda mfupi aliyumba na kujigonga ukutani na kuanguka chini.baada ya kuanguka, Lulu alikimbia na kwenda kujifungia chooni kwa hofu na baada ya muda alitoka na maji na kwenda kummwagia Kanumba lakini hakuamka.Alidai kuwa baada ya kuona hali hiyo alishikwa na hofu na kuamua kukimbia kwenye ufukwe wa Coco Beach. Alidai kuwa akiwa huko alipewa taarifa kuwa Kanumba amefariki na ndipo alipompigia simu rafiki yake ili aende kumsaidia kuendesha gari waelekee kwenye msiba (Haya ni maelezo yaliyotolewa mahakama ya kisutu )

 Uchunguzi wa awali wa polisi ulionyesha kuwa hakukuwa na jeraha lolote kuanzia kichwani hadi mwilini kwa Kanumba.

uchunguzi wa kifo hicho ulifanywa na jopo la madaktari watatu na daktari mmoja wa familia kutoka hospitali ya Amana ambapo ulibaini kuwa ubongo wa Kanumba ulikuwa umevimba na damu imevilia


Januari 29 mwaka 2013 Lulu aliachiwa kwa dhamana baada ya kesi hiyo kubadilishwa hati ya mashitaka kutoka kwenye kesi ya mauaji kwenda mauaji ya bila kukusudia ambapo badiliko hilo lilimpa nafasi ya kupata dhamana.


Katika kesi ya msingi inadaiwa kuwa Aprili 7 mwaka 2012 Sinza Vatican jijini Dar es Salaam, Lulu alimuua Kanumba bila kukusudia. Lulu atarudishwa katika Mahakakama Kuu Tanzania Kanda ya Dar es Salaam Februari 17 mwaka huu. Tumuombee aweze kushinda kesi hii.
Previous Post Next Post