January Makamba na Sugu Katika wimbo mmoja na wasanii wengine 13

Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba pamoja na Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi aka Sugu watasikika kwenye wimbo uitwao ‘Haki’ uliofanywa na wasanii 13 wa Hip Hip. Katika wimbo huo, January Makamba amefanya intro na Sugu kufunga na outro.


Wasanii walioshiriki kwenye Haki ni pamoja na Quick Rocker, Mchizi Mox, Godzilla, Kala Jeremiah, G-Nako na Nikki wa Pili. Wengine ni Fid Q, Joh Makini, Gosby, Profesa Jay, Mwana FA, Danny Msimamo na Kalapina.

Wimbo huo uliotayarishwa na P-Funk Majani kwenye studio za Bongo Records na utakaoachiwa Ijumaa hii, una lengo la kulihamasisha bunge la katiba mpya kuingiza suala la sanaa na haki za kazi za kiubunifu (Intellectual Property) kwenye katiba hiyo.

Previous Post Next Post