Zitto Kabwe Aishinda Nguvu kamati Kuu ya Chadema, Ashinda Rufaa yake

Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe ameibuka na ushindi baada ya mahakama kuu, jijini Dar es salam Jumanne hii kuamua kuwa mbunge huyo asijadiliwe na kamati kuu ya CHADEMA mpaka chama hicho kitaposikiliza shauri lake la kumvua uongozi ndani ya chama.

Zitto alipeleka shauri lake mahakamani ili kukitaka chama hicho kisijadili tuhuma zinazomkabili mpaka pale chama hicho kitaposikiliza shauri lake. Akizungumza na waandishi wa habari wakili wa Zitto Kabwe, Albert Msando amesema kamati kuu ya CHADEMA imeambiwa isijadili kitu chochote kuhusu uanachama wake.


“Tusubiri madai ya kesi ya msingi, hili la leo limepita salama,madai kwenye kesi ya msingi ni kwamba cha kwanza kamati kuu kupitia katibu mkuu wa chama impatie (Zitto )nyaraka ambazo zinatoa sababu na nyenendo wa shauri lake ambalo lilitumika kumvua nyadhifa zake za uongozi na pia kuagiza kamati kuu imchukulie hatua zaidi za kinidhamu kuhusiana na uanachama wake.

Baada ya kupatiwa nyaraka hizo ina maana atakuwa na nafasi ya kukata rufaa kwenye baraza kuu ambapo litamsikiliza kuona kama uamuzi wa tarehe 22 November 2013 wa kamati kuu ulikuwa sahihi. Hayo ndio madai ya msingi ambayo yapo kwenye shauri la msingi. Kwahiyo tarehe 13 April 2013 kesi itasikilizwa tena,” alisema Msando.

Tazama Picha hizi Chini Jinsi gani hali ilivyokuwa Mahakamani

Mwanasheria wa Chadema Tundu Lissu akisalimiana na Zitto Kabwe baada kukubaliwa ombi lake na mahakama
Zitto akitoka kwa msaada wa mabaunsa wake katika chumba cha mahakama kuu baada ya uamuzi huo wa Mahakama kuu leo jioni.

Tundu Lisu na wapambe wake wakionekana kutoka kwa aibu Mahakamani baada ya kubwagwa

 
Tundu Lissu akizungumza na wanachama wa CHADEMA nje ya mahakama baada ya kesi.

Wakili wa Zitto akizungumza na waandishi nje ya mahakama kuu.

 Wafuasi wa Chadema wanaomuunga mkono Zitto wakishangilia abaada ya ushindi wa kiongozi huyo

Wafuasi wa Chadema wanaomuunga mkono Zitto wakiwa wamekaa chini kutii amri ya polisi baada ya matokeo ya kesi kutangazwa upende wao ukiwa aumeibuka kidedea.

Wafuasi wa Chadema wanaounga mkono uongozi wa chama hicho kutaka Zitto atimuliwe uanachama, wakiwa wameduwaa nje ya mahakama baada ya uamuzi wa Jaji, John

Mmoja wa wafuasi wa Chadema upande wa wanaounga mkono uongozi akiwa amejeruhiwa kichwani baada ya kupigwa jiwe.

Mbwa mkali wa polisi akiwa tayari kwa lolote.
Wafuasi wa Chadema wakivurumishana mawe Zitto alipowasili mahakamani

 
Wananchi wa kawaida wakilazimika kusalimia maisha yao kwa kutimua mbio baada ya wafuasi hao wa Chdema kuanza kuvurumishiana mawe Zitto alipowasili Mahakama kuu
Previous Post Next Post