Makala: Dawa za kulevya na Mapinduzi ya viongozi zilivyoutikisa 2013

Zimesalia siku chache kabla ya kuuaga mwaka 2013 na kuanza mwaka mpya wa 2014, huku kukiwa na rekodi mbaya na nzuri katika sekta ya michezo.
Dawa za kulevya zilivyotikisa michezoni Miongoni mwa kumbukumbu mbaya ni kukamatwa kwa baadhi ya wanamichezo waliotuhumiwa kula njama na kusafirisha dawa za kulevya nje ya nchi.Juni 21: bondia Petro Mtagwa na wenzake watatu walihukumiwa kwenda jela miaka 15 baada ya kupatikana na hatia ya kula njama na kusafirisha dawa za kulevya aina ya Heroin nchini Mauritius walikokwenda kwenye shughuli za kimichezo.



“Mtagwa amenisonesha mno, nashindwa kula kila siku namlilia yeye, angalau hata angefungwa Morogoro au Dodoma, lakini nchi nyingine kabisa, sijui kama nitamuona tena,” alisema mama wa Mtagwa, Grace Mtagwa.Watanzania wengine waliohukumiwa kwenda jela nchini humo ni Case Ramadhani Fills, Nathanael Elia Charles na Ally Rajabu Msengwa ambapo jaji wa Mahakama ya Mauritius, Benjamin Marie Joseph alisema mahakama haina shaka na watu hao kukutwa na dawa hizo, hivyo kwa kuwa walishakaa mahabusu miaka mitano, watakaa gerezani miaka 10.

Hata hivyo bondia, Emmilian Patrick, kocha Nasoro Maiko na aliyekuwa rais wa BFT, Shaban Mintanga waliachiwa huru baada ya kukosekana ya kukosekana ushahidi wa kuwaona wana hatia., Mintanga alikuwa Dar es Salaam na Emmilian na Maiko walikamatwa Mauritius


Agosti 31:Mshambuliaji wa nyota wa zamani wa timu ya soka ya Simba na Taifa, Joseph Kaniki ‘Golota’ na bondia Mkwanda Matumla walikamatwa jijini Addis Ababa,


Ethiopia wakituhumiwa kusafirisha dawa za kulevya.Kaniki na Matumla walikamatwa Agosti 31, mwaka huu kwenye Uwanja wa Ndege wa Bole, Addis Ababa wakati wakijiandaa kupanda ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia tayari kwa safari ya kuelekea Paris, Ufaransa.Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia, Samuel Shelukindo alithibitisha wanamichezo hao kushikiliwa nchini humo na Polisi wa Kitengo cha Uchunguzi wa Makosa ya Jinai.

“Mkwanda ameifedhehesha familia, kama ni kweli kafanya kitendo hiki, ninachojua mimi alikuwa akifanya biashara zake,sikuwahi kufikiria kama anasafirisha dawa za dawa za kulevya,” anasema kaka mkubwa wa Mkwanda, Rashid Matumla ‘Snake Man’.


Cheka atwaa taji, Maugo azimishwaAgost 31: Bondia Francis ‘SMG’ Cheka alitwaa taji la dunia la WBF baada ya kumkung’uta Phil ‘The Drill’ Williams kwa pointi katika pambano la raundi 12 la uzani wa super middle kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam.


“Namaliza mwaka nikiwa na taji la ubingwa wa dunia wa WBF, ili ni miongoni mwa mataji yangu saba ya ubingwa ya taifa na Afrika ambayo nayashikilia hivi sasa,” anasema Cheka.


Mashali amzimisha Maugo: Usiku wa siku hiyo, bondia Thomas ‘Simba asiyefugika’ Mashali alizima ‘ngebe’ za hasimu wake Mada ‘King’ Maugo baada ya kumkung’uta

kwa pointi japo Maugo alipingana na matokeo na kudai mpinzani wake kabebwa.Kabla ya pambano hilo, Maugo alimwambia Mashali hawezi ngumi, akaombe kazi ya kupika chapati hotelini wakati Mashali akimfananisha Maugo na mdori.
Bondia azamia Australia

Novemba 17: Bondia wa Tanzania, Jonas Segu alizamia nchini Australia alipokwenda kuzichapa na Luke Sharp kwenye jimbo Northbridge, na Segu kupigwa kwa Knock Out (KO) raundi ya tano kwenye uzani wa light welter.Muda mfupi baada ya Segu kushuka ulingoni na kulipwa fedha zake hakuonekana tena na hakuwa kwenye msafara wa wachezaji wa Tanzania waliokwenda kuzichapa nchini humo wa kurudi nchini.Aliyekuwa mkuu wa msafara wa timu hiyo ya Tanzania, Obote Ameme alithibitisha bondia huyo kuzamia nchini


humo na kueleza kuwa walifanya juhudi za kumtafuta na kutoa taarifa kwenye vyombo vya habari vya nchi hiyo bila mafanikio. Familia ya Segu inayoishi Mburahati Dar es Salaam haikuwa na cha kufanya baada ya kubaini ukweli kuwa kijana wao alizamia nchini humo na kudai inamwachia Mungu.


Tenisi ilifanya mapinduzi ya viongoziAprili Mosi:Baadhi ya wajumbe wa Chama cha Tenisi Tanzania wakiongozwa na Kiango Kipingu walianza kampeni ya kuuondoa madarakani uongozi wa aliyekuwa Katibu Mmkuu Inger Njau.


Wiki chache baadaye Inger aliandika barua ya kujiuzudhurulu kabla ya Juni 22 chama hicho kufanya uchaguzi mkuu uliowaweka madarakani Methusela Mbajo kuwa rais, Fina Mango makamu wake na William Kallaghe kuwa katibu mkuu.

Toa maoni yako Kuhusiana na Makala Hii
Previous Post Next Post