Diamond Plutnumz na Davido kwa nini waliamua kufanya Collabo Moja?

Katika harakati ya kufanya muziki uendelee level za juu kabisa na kuanza kuuza international basi ni vizuri kuanza hapa hapa nyumbani,then kama baadae flani hivi mambo yataanza kuji-set yenyewe na kukaa kwenye mstari. Kama ilivyo kwa msanii wa hapa Tzee Diamond platinumz naye alienda huko West Africa pande za Nigeria akiwa amemsimamisha msanii mkali anayekula airtime huko nchini kwao , Davido kwenye remix yake ya mynumber1.


Davido baada tu ya kuona nyimbo aliyopiga collabo na msanii huyu wa Tz ,Diamond Platnumz na kuzidi kufanya vizuri sana Africa,ameona kuwa hivi sasa aendeleze mashambulizi ya kufanya collabo na wanamuziki wanao-hit nchi mbali mbali za Africa. Diamond akiwa ndio kama amefungua dimba katika safari yadavido kufanya na kuendeleza collabo za wasanii nje ya West Africa na yeye amezidi kupanga mikakati ya kufanya collabo nyingi zaidi na wasanii wengi wakubwa hapa africa.

Baada tu ya kufanya collabo na Diamond Platnumz na video yake kufanya vizuri sana duniani ambapo mbali na africa huonyeshwa katika television za nchi za nje na inasemekana imeingia katika moja list ya nyimbo kali za Africa,wasanii wengi wameonekana kutaka kufanya collabo nae ili nao waweze kufika mahali fulani pazuri,huku davido nae bila kupoteza chance nae kutafuta wa kwake katika harakati ya kuchanganya ladha ya muziki wa aina tofauti ili uweze kuuzika zaidi nchi tofauti,hadi hivi sasa ameshafanya collabo na msanii maarufu kutoka nchini Uganda, Dr Josse Chameleon,D’banj wa nigeria na kuvuka hadi south africa kufanya collabo na wakali wa khona aka mafikizolo.

Davido akiwa na kundi la mafikizolo

Kama ilivyo kwa wasanii wengine wengi waliopita wakiwemo Psuare ,D’banj na wengineo wengi,wamepitia njia hii hii moja ya kufanya colllabo na watu wengi wanao-hit hapa Africa hadi kuweza kusikika nje ya mipaka ya africa na kuweza kufanya collabo na wasanii wakongwe Marekani na Ulaya,ni moja ya mbinu inayoaminika kuzidi kufanya kazi,kwa msanii kufanya vizuri na kufikia malengo yake ya kuweza kuuza kazi zake international zaidi.

Previous Post Next Post