Picha: Club ya Mpira wa Miguu ya Azam Yapata Usafiri wa Kisasa Tazama Hapa

Club ya mpira wa miguu ya hapa jijini Dar-Es-Salaam ya Azam imeamua kubadilisha usafiri wa basi la zamani lililokuwa likitumika kusafirisha wachezaji wake na crew nzima ya timu hiyo, na kuagizia basi jipya ambalo ni la kisasa zaidi lililowasili jijini Dar tarehe 28 mwezi huu. Basi hilo ndani linakaribia kuwa na kila kitu; ikiwemo choo, friji na Tv katika kila siti kama yale mabasi makubwa yanayotumiwa na timu kubwa za nje.


Wakati timu ya Azam ikiwa katika maandalizi kwa ajili ya kushiriki shindano la Mapinduzi visiwani Zanzibar … basi hili limesafirishwa huko Zanzibar kwa ajili ya matumizi rasmi ya club hiyo …

 Basi Hilo la Azam kwa Ndani jinsi linavyoonekana

Choo Kidogo Ambacho kinpatikana ndani ya Basi hilo la Azam
Previous Post Next Post

Popular Items