Penzi la meneja wake lampagawisha baby Madaha, aamua kufunguka haya

Baby Madaha ambaye star wa bongo movies na pimwanamuziki wa Bongofleva amesema kuwa mpenzi wake wa sasa Joe Kariuki kutoka nchini Kenya ambaye pia ni meneja wake na pedeshee wa label ya Candy n Candy anamkoleza sana kimapenzi na hawezi kumuacha kamwe bali anatamani ahamie nchini Kenya kabisa.


Akizungumza na Globalpublishers Madaha anayetamba na wimbo wa Summer Holiday kwasasa alisema "Kusema kweli huyu kaka kanikoleza jamani japo watu watachonga mengi lakini abadani sitosikiliza maneno yao, kwa kuwa awali sikuwa na uhusiano naye ila porojo za watu zilipelekea kuchukua maamuzi hayo natamani niamie Kenya ili tuwe karibu wakati wote". Alisisitiza baby Madaha. 


Source:BongoMovies 

Previous Post Next Post