Orodha yao ya nyimbo 10 za Tanzania zilizofanya vizuri mwaka 2013 Iliyotolewa na Sppoti Starehe

Gazeti la Spoti Starehe limetoa orodha yake ya nyimbo 10.Katika orodha hiyo nafasi ya kwanza imekamatwa na wimbo wa Diamond Platnumz, My Number One.



“Video ya wimbo huu imepata watazamaji zaidi ya 1.5 milioni tangu ulipowekwa You Tube kwa mara ya kwanza mwezi Septemba. Ni wimbo ulioweza kumtambulisha Diamond kimataifa,” limeandika gazeti hilo.

“Alirekodi katika studio ya kawaida sana, Burn Records, lakini wimbo huo umeweza kumkutanisha na mastaa wakubwa barani Afrika. Kwa mara ya kwanza ameweza kufanya kolabo na Davido, Iyanya na wanamuziki wengine mashuhuri barani Afrika. Ameweza kutambulika kimataifa kutokana na video hiyo kuonyeshwa katika televisheni nyingi Afrika sambamba na mahojiano.”

Nafasi ya pili imekatwa na single iliyomtoa Young Killa, ‘Dear Game’.

“(Young Killer) amepata shoo nyingi, ni kijana mdogo aliyeibukia katika Super Nyota 2012. Ameweza kuliteka soko na kupata shoo nyingi zilizomwingizia kipato kikubwa,” limeandika.

Kwenye nafasi ya tatu, yupo Ommy Dimpoz na Tupogo, nafasi ya nne ikienda kwa AY na FA na wimbo wao Bila Kukunja Goti waliomshirikisha J-Martins huku nafasi ya tano ikienda kwa Nay wa Mitego na Diamond na wimbo wa Muziki Gani.

Nafasi ya sita imekamatwa na Yahaya ya Lady Jaydee, ikifuatiwa na Majanga ya Snura kwenye nafasi ya sababu, Roho Yangu ya Rich Mavoko imekamata nafasi ya nane, Salam Zao ya Nay wa Mitego nafasi ya 9 na Utamu ya Dully Sykes, Ommy Dimpoz na Diamond ikikamata nafasi ya 10.
Previous Post Next Post